Chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) kimeiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa watu wanaokutwa na hatia ya kuwakata viungo au kuwaua watu wenye Ualbino.
Hayo yamesemwa leo Juni 12, 2024 mjini Kibaha na Mwenyekiti wa TAS Taifa Godson Mollel alipozungumza na waandishi wa habari wakati wa Kongamano la kuongeza uelewa juu ya Ualbino duniani katika ukumbi wa Chuo cha Uongozi Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha kwa Mfipa.
Mollel amesema kuwa Mahakama ikotoa hukumu kali kwa wahusika hao itakuwa fundisho kwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha kuwadhuru watu wenye Ualbino.
Naye Afisa ustawi mkuu toka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Watu wenye ulemavu Joy Maongezi amesema kuwa sheria namba 9 ya mwaka 2010 inataka kuwa na haki kwa watu wenye ulemavu ambapo watu wenye Ualbino ni sehemu yao.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Shangwe Twamala amesema kuwa wakati wa maadhimisho hayo huduma mbalimbali zinatolewa ikiwa ni pamoja na upimaji saratani ya ngozi, utoaji miwani, kofia na vilainishi (losheni) ya kuzuia ngozi kuathirika, upimaji wa tezi dume na kansa ya kizazi.
Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka duniani ambapo kilele huwa tarehe 13 Juni kila mwaka na kwa mwaka huu kitaifa yanafanyika Kibaha Mkoani Pwani.mo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.