Serikali Mkoani Pwani imesaini waraka wa makubaliano ya awali ya ushirikiano na jimbo la Fujian la nchini China katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi,uwekezaji, afya na elimu.
Uwekaji wa saini hiyo ya makubaliano ya awali ya ushirikiano huo, umefanyika katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Pwani baina ya Mhandisi Evarist Ndikilo na makamu mwenyekiti wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CCP)kutoka jimbo la Fujian Pan Zheng .
“Kwanza tumesaini makubaliano ya awali ya ushirikiano kati ya Mkoa wa Pwani na Jimbo la Fujian katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Viwanda,Elimu,Afya pamoja na kubadilishana uzoefu mbalimbali.Makubaliano hayo ya awali yatawasilishwa kwa serikali ya jimbo la Fujian ambapo itatoa fursa kwa wafanyabiashara kuangalia namna Pwani ilivyojipanga kwenye sekta ya uwekezaji” alisema Mhandisi Ndikilo. .
Aidha mhandisi Ndikilo alisema kuwa,Mkoa wa Pwani umepata mwaliko wa kwenda kushiriki maonesho yatakayofanyika katika Jimbo la Fujian ,mwezi Septemba mwaka huu ,ambayo yataurahisishia Mkoa wa Pwani kutangaza fursa zilizopo Mkoani humo.
Katika Hatua nyingine Makamu mwenyekiti wa Jimbo la Fujian Pan Zheng ameipongeza Serikali ya Mkoa wa Pwani kwa namna ilivyojipanga kuwavutia wawekezaji na kusema kuwa Mkoa utaendelea kupata wakezaji wengi zaidi kwa sababu ya Fursa zilizopo Mkoani Pwani ambazo zinawavutia kuwekeza katika maeneo mbalimbali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.