WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amezielekeza Jumuiya za maji kuzingatia utaratibu wa kupeleka fedha benki ambao utasaidia miradi hiyo kuwa endelevu.
Ameyasema hayo alipokuwa akizindua mradi wa maji katika kata ya Chumbi Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani uliojengwa kwa usimamizi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) na kugharimu sh. milioni 722.
Katika maelekezo hayo, Waziri Aweso ameziambia Jumuiya za watumiaji maji ambao wanasimamia mradi huo wa Chumbi kuhakikisha kuwa fedha wanazokusanya zinawekwa benki ili mradi uwe endelevu.
"Nimekuwa nikishuhudia baadhi ya Jumuiya wananchi wanakusanya fedha baadae viongozi wao wanagawana kwa kupokezana na inapotokea mmoja wa wajumbe kukosa huanzisha ugomvi unaosababisha kuvunjika Jumuiya husika, hivyo, nataka niwaambie vipo vya kuchezea sio fedha za miradi ya maji, tutashighulikiana," amesema.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali inayotatua kero za Wananchi.
Kunenge amesema mradi huo unakwenda kuondoa kero ya wananchi kutumia muda mwingi kusaka maji.
Mradi wa maji Chumbi ambao umeanza kutumika unatarajia kuhudumia zaidi ya wakazi 8000 wa Vijiji vya Chumbi A, B, na C
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.