Wiki ya Uwekezaji na Biashara Mkoani Pwani,inatarajia kufanyika octoba 5-10 mwaka huu ,ikiwa ni maonyesho ya tatu tangu kuanzishwa kwa maonyesho hayo mwaka 2018.
Katika maonyesho hayo washiriki 520 wanatarajia kushiriki moja kwa moja na watu 15,000 watatembelea kujionea bidhaa zinazozalishwa kupitia viwanda na fursa zinazopatikana Mkoani humo.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhe. Abubakari Kunenge, akizungumza na waandishi wa habari Mkoani hapo kuhusiana na maonyesho hayo ,aliwaeleza kwamba yatafanyika kwa ushirikiano na Shirika linalohudumia viwanda vidogo vidogo( SIDO )Kanda ya Mashariki na TANTRADE wanashughulika na uratibu ambapo yatafanyika katika Viwanja vya Stendi ya zamani Mailmoja Kibaha Mjini .
Alieleza ,awali maonyesho hayo yalikuwa yafanyike September 14-19 Lakini kutokana na Zoezi la sensa waliona kusiwe na muingiliano hivyo kutumia nguvu zote kufanikisha Zoezi hilo muhimu la Kitaifa.
Vilevile,watakaotembelea maonyesho wataenda kutembelea kongani za viwanda kuona namna mkoa ulivyojinabu kupitia sekta hiyo.
Kunenge alielezea ,pia kutakuwa na kongamano la uwekezaji ambalo litaonyesha fursa za viwanda na uwekezaji Mkoani Pwani.
"Mkoa kwa sasa una zaidi ya viwanda 1,460 kati ya hivyo 90 ni vikubwa na kila siku idadi inaongezeka, Tunawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza "
"Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kuweka msukumo katika kuvutia wawekezaji nchini,Na tukio hili linakwenda kutafsiri kwa vitendo namna tunavyounga mkono juhudi za Serikali"alifafanua Kunenge.
Akizungumzia suala la TIN number ili kuongeza mapato ya mkoa alisema ,kwasasa wanadhibiti wenye viwanda Kuwa na Namba hizo mkoa wa Dar es salaam ambapo awali walikuwa wakinufaisha mkoa mwingine wakati wakiwa wamewekeza Mkoani hapo.
"Tuna Taasisi 17 ambazo tunashirikiana nao kusikiliza kero za wawekezaji na kuboresha Mji wetu,Nimeseme tuu katika maongezi yetu yanazaa matunda wengi wanalipa na kufanya usajili Mkoani kwetu, ngazi ya mkoa tunalifanyia kazi na linaleta tija ,"alisema Kunenge.
Hata hivyo ,alisema kwasasa wanapanga Maeneo mbalimbali ya mkoa Kuwa Mji wa kisasa ikiwemo Mji wa Kwala ,kupanga kisiwa cha Mafia ,suala hili ni la muda na michakato inaendelea.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.