#Kwa mara ya kwanza Serikali katika mwaka wa fedha 2017/2018 imetenga kiasi cha Bil.11 kwaajili ya kufanikisha masuala ya Lishe ikimaanisha kila mtoto ametengewa tsh.1000, nawasihi wakuu wa mikoa tukasimamie hili kwa karibu. Mh. Jafo
#Kupitia Mitandao ya Kijamii kama Blog na tovuti Mh. Rais anafatilia na anaona kazi kubwa mnayofanya, Mh. Rais, lakini pia Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wanatambua kazi kubwa mliyo nayo nawasihi tuendelee kufanya kazi. Mh. Jafo
#Hali ya Lishe Duni imetamalaki nchini ambapo Udumavu ni asilimia 34.4, Uzito mdogo asilimia 4.5 na Ukondefu asilimia 13.5 hili ni jambo zito sana lazima tuwe na Nguvu ya Pamoja. Mh. Jafo
#Maelekezo ya Makamu wa Rais tusaini Mikataba na tukasimamie suala la Lishe kiufasaha kwani viongozi wetu wa awamu ya tano wanaimani kubwa sana na timu hii ya Wakuu wa Mikoa. Mh. Jafo
#Fedha hizi zilizotengwa hazitakuwa kwa Mkuu wa Mkoa, hivyo kawaelekezeni Wakurugenzi na kuwasimamia juu ya fedha zilizotengwa zikafanye kazi iliyokusudiwa hususani masuala ya lishe. Mh. Jafo
#Watendaji katika Maeneo yenu, Muwaelekeze ili wawashauri wamama wajawazito kutumia Folifolic acid ili kupunguza tatizo la Lishe duni. Mh. Jafo
#Tumetenga Bil .256 kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi katika bajeti ya mwaka 2017/2018 Mh. Jafo
#Tumefanikiwa kuanzisha mfumo wa kieletroniki wa GoTHoMIS wa Ukusanyaji wa taarifa na udhibiti wa mapato katika vituo vya Afya vilivyo chini ya Mikoa na Mamlaka za serikali za Mitaa. Mh. Jafo
#Wizara imefanikisha upatikanaji wa fedha za kugharamia ujenzi na upanuzi wa vituo vya Afya 2011 kuwezesha huduma za dharura kwa wajawazito. Mh. Jafo
#Tumefanikiwa kuajiri Wahasibu wasaidizi 535 kwa ajili ya vituo vya afya Nchini. Mh. Jafo
#Tumefanikiwa kuongeza wigo wa mpango wa Malipo kwa Ufanisi (RBF) kutoka Mkoa mmoja mwaka 2016 hadi Mikoa 8 katika mwaka, 2017. Mh. Jafo
#Tumefanikiwa kuwaajiri Madaktari 206 waliokuwa wameomba kwenda kufanyakazi nchini Kenya na kuajiri watumishi wengine wa kada za Afya wapatao 3,152. Mh. Jafo
#Tunawapongeza kwakutumia Force Accout, ambapo kote nilikopita nimeona jinsi kazi inavyokwenda wengi wapo kati ya asilimia 70, 80 hadi tisini na kitu, nimatumaini yangu ile tarehe 30 Desemba, 2017 tuliokuwa tumejiwekea tutakuwa tumekamilisha kazi ya ujenzi. Mh. Jafo
#Tumeamua kutumia Force account kwasabu moja kubwa, kwanza kuondosha urasimu ulikuwepo lakini Majengo hayakuwa na Viwango lakini pia kuinua uchumi wa wananchi wetu na kwakweli wanafanya kazi nzuri sana. Mh. Jafo
#Jambo lakipaumbele kwa Wakurugenzi Bil. 20 ikatumike na tusije kusikia fedha imeenda kwenye Bakaa, wapo DMOs waliotukwamisha huko kipindi kilichopita kwakweli hatukumvumilia na hata atakaye tukwamisha hatuwezi kumvumilia atapewa majukumu mengine anayo yaweza. Mh. Jafo
#Wakurugenzi Watoe taarifa kwa Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Wilaya Waziwasilishe kwa Mh. Mkuu wa Mkoa zaidi ya yote Mkuu wa Mkoa awe na (ownership) ya miradi yote iliyopo katika Mkoa wake hata wanapokuja wageni wa Kitaifa wawe na nafasi nzuri yakuisemea wakati wa utoaji wa taarifa. Mh. Jafo
Imeandaliwa na
OR - TAMISEMI
DODOMA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.