• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

Dawa sasa kuzalishwa Pwani

Posted on: April 4th, 2018

Mkoa  Pwani, umetekeleza  wito wa serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli   wa kujenga viwanda vya madawa na  vifaa tibana Vitendanishi  ambapo inatarajia kuwa na viwanda  vitatu, hali ambayo itaondoa  adha ya kuagiza madawa  kutoka nje ya nchi , na  imekemea tabia inayofanywa na baadhi ya wawekezaji ya kutoa ajira kwa watu kutoka nje ya nchi na kuwanyima  fursa hiyo wananchi wa  Pwani na Watanzania kwa ujumla

.
Akielezea masuala ya uwekezaji na ajira ,wakati wa ziara yake ya kutembelea viwanda mjini Kibaha ,Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Mhandisi Evarist Ndikilo alisema Viwanda vya madawa vitawezesha kuokoa mamilioni ya fedha yaliyokuwa yakitumika kununulia madawa kutoka nchi za nje.
Alieleza kuwa viwanda vitatu vinavyojengwa  Mkoani Pwani ni pamoja kiwanda cha Kairuki Pharmaceuticals Industry Ltd ,Zinga Pharmaceuticals ambacho kitajengwa kwa ubia na  Israel  na kipo mbioni kuanza kujengwa na kiwanda cha Bahari Pharmaceuticals .
“Tumeitikia  wito wa Rais Dk.John Magufuli ,lakini pia tangu kipindi cha nyuma tumejipanga kujenga viwanda hivyo ,kupitia ziara hii tunawathibitishia wananchi tunaunga mkono kauli ya serikali yetu”alisema Mhandisi Ndikilo.
Pia alieleza kuwa ,zipo fursa mbalimbali za uwekezaji lakini vijana na wazawa wanashindwa kukimbilia fursa hizo.
Ndikilo alisema wazazi na vijana bado hawajatambua kujipanga kukuza elimu na ujuzi wao kwa ajili ya kujipatia ajira kirahisi na alitoa rai kwa wawekezaji ,kuacha kuwanyima ajira wazawa na watanzania ambao wanaujuzi na sifa za kufanya kazi .
” Haiwezekani tunajenga viwanda vingi lakini vijana ,waTanzania  hasa kutoka Pwani hawanufaiki na ajira zinazopatikana, suala hili haikubaliki na sidhani kama Pwani ama Tanzania nzima haina wenye sifa na ujuzi unaotakiwa ,hivyo aliwataka wawekezaji hao watoe kipaumbele kwa watanzania wenye uwezo .
Ndikilo aliongeza kusema kuwa, amepokea taarifa ya ujenzi wa reli ya  Standard Gauge eneo la Soga hawatoi ajira hata ya udereva jambo ambalo analichunguza na atakapopata uhakika watachukua hatua zinazostahili.

Aidha Mh Ndikilo alionyesha masikitiko makubwa  kutokana  na taarifa kuwa  mkandarasi wa ujenzi wa kiwanda cha  Kairuki  Pharmaceutical Industry   anaagiza vifaa vya ujenzi kama  nondo  kutoka Uturuki kwa madai kuwa nondo zinazozalishwa  hapa nchini  hazina ubora.

Ndikilo alisema  kuwa vipo viwanda  vinavyozalisha nondo zenye ubora mfano kiwanda cha Kiluwa Investment kilichopo Mkoani Pwani hivyo  akawataka kuanzia sasa   wanunue nondo katika viwanda vilivyop ndani ya nchi.
Nae mkurugenzi mtaalamu wa Kairuki Pharmaceuticals Mhandisi.Valency Assenga alisema ujenzi wa mradi huo ulianza Machi 10 mwaka huu na mkandarasi ni Petra Construction Ltd Ltd na unatarajiwa kumalizika Novemba 2018.
Alielezea kuwa  kazi zote zinaendelea vizuri na  zipo katika hatua ya awali ya ujenzi  ambapo kazi hiyo inatarajiwa kugharimu jumla ya fedha za kitanzania shilingi  bilioni 3.9 kwa awamu ya kwanza.  
Mhandisi .Assenga alitaja changamoto zilizopo kuwa ni miundombinu ya barabara,mradi kusuasua kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na ucheleweshwaji wa uunganishwaji wa umeme.
Katika Hatua nyingine nae Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kibaha, Bi Jennifer Omolo akizungumzia suala la mipango miji alisema wameanza zoezi la kupima Mji muda mrefu na wanaendelea na zoezi hilo .
Pia aliwataka watu waache kujenga na kufanya biashara kiholela bila kupangwa ,na kuwashauri waone watalaamu wa mipango miji Ofisi ya Mkurugenzi ili kupewa maelekezo ya kupata vibali vya ujenzi .

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RS Pwani Yaibuka Kidedea kwa Ushindi wa "-1 Dhidi ya Kibaha TC

    May 01, 2025
  • Rais Samia Apongezwa kwa kuwa Kiongozi wa Mfano katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mkoani Pwani

    May 01, 2025
  • RC Kunenge Aagiza CORECU Kutekeleza Maomo ya Rais Samia Kuhusub Ushirika

    April 30, 2025
  • Spika Tulia Asisitiza Umuhimu wa Muungano katika kuimarisha Umoja na Amani

    April 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.