• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

Dkt Jakaya Kikwete Kuwa Mgani rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya Uwekezaji na Biashara Pwani :RC Kunenge

Posted on: October 5th, 2022

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Wiki ya maonesho ya Kimataifa ya uwekezaji na Biashara yatakayofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani vilivyopo Mailimoja Kibaha Mjini.

Maonesho hayo yataanza Oktoba 5 na kumalizika Oktoba 10 ambapo wadau mbalimbali watashiriki ikiwa sehemu ya kuonyesha bidhaa zinazozalishwa katika viwanda vilivyopo Mkoani Pwani.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe  Abubakari Kunenge,ametoa taarifa hiyo leo awakati akizungumza na Waandishi wa habari katika viwanja hivyo ikiwa sehemu ya kuhamasisha wawekezaji,Wafanyabiashara,wadau na wananchi kushiriki maonesho hayo.

Kunenge ,amesema kuwa maandalizi ya shughuli nzima mpaka sasa yamekamilika kwa asilimia 95 na kwamba bado wadau wanakaribishwa kushiriki kwakuwa fursa ipo wazi kwa ajili yao na kwamba mpaka sasa tayari wawekezaji 200 wamethibitisha kushiriki.

"Wiki ya maonesho ya Uwekezaji na Biashara yataanza kesho Oktoba 5 lakini ufunguzi mi utafanyika Oktoba 6 na mgeni wetu rasmi ni Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete," amesema Kunenge

Aidha Kunenge ,amesema kuwa katika wiki hiyo yapo mambo mbalimbali yatafanyika ikiwemo Kongamano kubwa la wawekezaji litakalofanyika Oktoba 10 katika Chuo Cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kilichopo Kibaha kwa Mfipa.

Amesema, Kongamano hilo litahudhuriwa na wawekezaji mbalimbali ,wataalamu wa kiuchumi, viongozi wa Serikali na taasisi wezeshi huku akiwaomba wananchi wajitokeze kushiriki kongamano hilo ili wapate fursa ya kujua maeneo ya uwekezaji yaliyopo katika Mkoa .

Amesema,lengo kubwa la maonesho hayo ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akifanyakazi kubwa kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ya wawekezaji.

Kunenge, ameongeza kuwa kupitia maonesho hayo wananchi watapata fursa ya kujionea bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya Mkoa wa Pwani,kupata fursa mpya za uwekezaji , wazalishaji. kupata masoko ya uhakika,kujua teknolojia za kisasa.

"Pamoja na faida kuwa nyingi katika maonesho haya ,lakini pia itakuwa fursa kubwa ya kuona jinsi gani sera nzuri na jitihada za Rais zinavyoweza kutoa majibu juu ya masuala ya uwekezaji hapa nchini ,amesema Kunenge

Ameongeza kuwa , maonesho hayo yataonyesha namna ambavyo wawekezaji wa Mkoa wa Pwani walivyopiga hatua ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya nchi katika uwekezaji.

Amesema, maonesho hayo yanatoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo na kwamba amewataka wakazi wa Mkoa wa Pwani kutumia fursa hiyo kufanya biashara ili wajiongezee kipato.

Hatahivyo, Kunenge amewaomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika maonesho hayo ili kuona kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RS Pwani Yaibuka Kidedea kwa Ushindi wa "-1 Dhidi ya Kibaha TC

    May 01, 2025
  • Rais Samia Apongezwa kwa kuwa Kiongozi wa Mfano katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mkoani Pwani

    May 01, 2025
  • RC Kunenge Aagiza CORECU Kutekeleza Maomo ya Rais Samia Kuhusub Ushirika

    April 30, 2025
  • Spika Tulia Asisitiza Umuhimu wa Muungano katika kuimarisha Umoja na Amani

    April 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.