Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Salma Maghimbi amewaasa Viongozi na Wajumbe wa Kamati ya Maadili ya Maofisa wa Mahakama kuhakikisha wanashughulika na malalamiko kwa kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu husika na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia mipaka waliyowekewa kisheria.
Jaji Maghimbi ameyasema hayo wakati akiwaapisha Viongozi na wajumbe wa Kamati ya Maadili ya Maofisa wa Mahakama wa Mkoa wa Pwani katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa huo mjini Kibaha ambapo pia amewaasa Viongozi na Wajumbe wa Kamati kuzingatia kiapo chao kwa kutunza siri na kutofanya upendeleo katika utekelezaji wao wa majukumu.
pamoja na kushughulikia malalamiko ambayo kanuni zimeelekeza bila kujadiliwa na kamati,"alisema Maghimbi.
Hayo yalisemwa zi ya Mkoa.
"Kazi hii inahitaji usiri, kutokuegemea upande wowote ikimaanisha bila kuwa na upendeleo, huba wala chuki kwa upande wowote ule kama kiapo kinavyoonyesha na kusimamia ukweli uliopatikana katika uchunguzi," amesema na akaongeza, "bila kufanya hivyo kama uchunguzi haukuwa wa haki mnaweza mkasababisha matatizo makubwa kwa Hakimu anayechunguzwa na hata kusabisha kufukuzwa kazi, jambo la muhimu la kuwakumbusha kila mmoja kuyazingatia aliyoapa kwa kumtanguliza Mungu ili haki iweze kupatikana kwa kila mmoja wenu kulingana na imani zenu za dini."
Amefafanua kuwa mara kwa mara wahusika wanaofikisha kesi zao mahakamani ni wananchi au wawakilishi wa idara mbalimbali za serikali na watu binafsi, hivyo akaonya kuwa inawezekana kupitia hao, kwenye masuala ya kimaadili, kukawa na malalamiko mbalimbali yanayowahusu Mahakimu.
"Kwa muktadha huo na kwa vile sote tunajua kuwa si malalamiko yote ya Mahakimu yanayojadiliwa na vikao hivi, ni jukumu la Kamati kuhakikisha linachambua na kubaki na malalamiko yale tu ambayo yanatakiwa, na hapa ninawasisitiza kuwa kueni makini sana na masuala hayo," ametahadharisha Jaji Maghimbi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo Abubakar Kunenge amesema kuwa watakuwa makini na kutenda haki kulingana na uwezo wao na vipawa walivyopewa na Mungu ili wasijekuwajibishwa endapo watakiuka maadili na kuwa Kamati itasaidia pale ambapo wananchi wataona hawajatendewa haki, na kuhusu maadili Mkuu huyo wa mkoa ametumia fursa hiyo kuwahimiza kuyafikisha kwenye kamati hiyo ili sheria ifuate mkondo wake na haki ipatikane.
Naye Sheikh Hamis Mtupa ambaye ni mjumbe wa Kamati hiyo amesema kuwa watasimamia uadilifu na kutenda haki na kuzingatia kiapo walichokiapa huku Mchungaji Julius Shemkai akisema kuwa hawatakuwa tayati kumwonea mtu na wanamwomba Mungu awasaidie ili waweze kutenda haki wakati wakutimiza majukumu yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.