• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

Kaimu Katibu Tawala Msaidizi atoa wito kwa jamii Kuwalinda Watoto na Kuhakikisha malezi bora

Posted on: June 16th, 2025

Kaimu Katibu Tawala Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mkoa wa Pwani, Peter Billa, amewataka wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuwa walinzi wa watoto kwa kuhakikisha wanalelewa katika mazingira salama na bora.

Billa ametoa wito huo leo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Rashid Mchatta, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika kimkoa katika Shule ya Msingi Kambarage, Kata ya Tumbi, Halmashauri ya Kibaha.

"Yote yaliyosemwa hapa leo ni muhimu sana kwa ustawi wa watoto wetu. Mtoto anahitaji ulinzi na mazingira bora ya kuishi. Ni wajibu wetu sisi wazazi, walezi na jamii kuhakikisha hilo linatimia," alisema Billa.

Aidha, aliwasihi wazazi kuepuka migogoro isiyo ya lazima na matumizi ya lugha chafu au vitisho mbele ya watoto kwani hali hiyo huharibu afya ya kisaikolojia ya mtoto na kuathiri mwenendo wake shuleni. Alisisitiza umuhimu wa wazazi kuwa karibu na watoto ili kutambua changamoto zinazowakabili, hususan masuala ya ukatili wa kijinsia.

Billa pia aliwataka wazazi na watoto kushiriki ibada na kuepuka kujihusisha na shughuli zisizofaa mitaani kama vile vibanda umiza, akisisitiza kuwa kushiriki katika imani za kidini hujenga maadili na kuwapa watoto misingi ya kukataa kushiriki vitendo viovu.

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Pwani, Grace Tete, alisema maadhimisho hayo yalitanguliwa na kampeni mbalimbali za kuelimisha jamii kuhusu haki za watoto. Kupitia kampeni hizo, zaidi ya wazazi na walezi 2,000 walifikiwa kwenye maeneo ya masoko mbalimbali mkoani humo.

Aidha, alieleza kuwa Serikali kupitia Mpango wa Taifa wa Kuzuia Ukatili dhidi ya Watoto, imefanikiwa kuwafikia watoto 150 waliopata madhila ya ukatili na kuwapatia huduma stahiki.

Tete alisisitiza kuwa wazazi na walezi wanapaswa kutimiza mahitaji ya msingi ya watoto kama vile chakula, malazi na elimu ili kuwalinda dhidi ya vishawishi hatarishi. Pia alihimiza jamii kuhakikisha mawasiliano bora kati ya watoto na walezi kwa lengo la kujua mapema matatizo yanayowakabili watoto.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Diwani wa Kata ya Tumbi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Lubawa, aliipongeza Polisi kwa kuimarisha ulinzi na kukabiliana na vitendo vya ubakaji na ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto katika kata hiyo.

Nao watoto, kupitia maonesho mbalimbali waliyoyafanya ikiwemo Bunge la watoto, ngonjera, mashairi na risala, waliwasihi wazazi kutimiza majukumu yao ipasavyo, kuepuka migogoro ya kifamilia na kulinda watoto dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa mwaka 2025 ni "Haki za Mtoto:Tulipotoka, Tulipo na Tuendako”. Kaulimbiu hii inaitaka jamii kutafakari upatikanaji wa haki za watoto tangu zilipoainishwa na Sera ya Maendeleo ya Mtoto mwaka 2008.

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kaimu Katibu Tawala Msaidizi atoa wito kwa jamii Kuwalinda Watoto na Kuhakikisha malezi bora

    June 16, 2025
  • Kanal Kolombo azindua mnada wa ufuta, atoa onyo kali dhidi ya utoroshaji wa mazao

    June 12, 2025
  • Pwani waanza kampeni ya utoaji elimu kuhusu malezi na makuzi bora ya Watoto

    June 10, 2025
  • Madaktari Bingwa 64 wawasili Pwani kwa Huduma maalum chini Mpango wa Rais Dkt Samia

    June 09, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.