Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani na Skauti Mkuu wa Tanzania, Rashid Mchatta, amepokea majiko ya gesi 200 kutoka kwa Mheshimiwa Dkt. Alice Kaijage, Mbunge wa Viti Maalum – Wafanyakazi. Majiko hayo yametolewa kwa ajili ya kugawiwa kwa watumishi wapya wa ajira mpya katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani pamoja na Halmashauri tisa (9) za mkoa huo.
Makabidhiano hayo yalifanyika mwanzoni mwa wiki katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, na yalishuhudiwa na Mheshimiwa Abubakar Kunenge, Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Baada ya kupokea majiko hayo, Katibu Tawala Mchatta aliyakabidhi rasmi kwa Wakurugenzi wa Halmashauri husika pamoja na kwa baadhi ya watumishi wapya wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mchatta alisema kuwa matumizi ya majiko hayo ya gesi ni hatua muhimu kwa watumishi wapya kutumia nishati safi ya kupikia, sambamba na kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.