Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge, Julai 27, 2025, amefunga rasmi mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo Watumishi wa Halmashauri ya Kibaha, yaliyofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha kwa Mfipa. Mafunzo hayo yalilenga kuwaongezea maarifa na ufanisi katika kushughulikia changamoto na kero za wananchi.
Akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo, Mhe. Kunenge aliwataka watumishi hao kuendelea kutatua changamoto na kero za wananchi kwa ufanisi ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Alisisitiza kuwa si jambo la kufurahisha kuona wananchi wakipeleka malalamiko yao hadi Ikulu ilhali viongozi na watendaji wa serikali wapo katika maeneo yao.
Aidha, Mhe. Kunenge aliwakumbusha Watumishi hao kuwa wao ndiyo walioko karibu zaidi na wananchi, hivyo wanapaswa kuwahudumia kwa weledi, haraka na ufanisi. Aliwataka kuwa na utendaji unaogusa wananchi moja kwa moja, kuchapa kazi kwa bidii na kuhakikisha vipaumbele vyao vinaendana na Dira ya Taifa 2050, Ilani ya Chama cha Mapinduzi, mipango ya maendeleo ya taifa pamoja na maelekezo ya Mhe. Rais.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.