• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

Mwenge wa Uhuru 2019 wazindua Mradi wa maji wqenye thamani ya Million 359,9 Kibaha.

Posted on: July 29th, 2019

Mwenge Wa Uhuru 2019 ,umezindua mradi wa maji katika kata ya Muheza,Mjini Kibaha ,Mkoani Pwani wenye thamani ya milioni 359.5, ambao chanzo chake cha maji ikiwa ni mto Ruvu kupitia DAWASA,huku ukitarajiwa kunufaisha wakazi 2,541.

Mhandisi wa maji halmashauri ya mji huo,Grace Lyimo alimweleza kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa,Mzee Mkongea Ali kuwa ,mradi huo ni mkombozi kwa wakazi hao.

Aidha alisema kuwa mradi huo ni kati ya miradi iliyopo chini ya programu ya Taifa ya maji na usafi wa mazingira vijijini ambapo ulichelewa kukamilika kutokana na uhaba wa fedha.

Grace alieleza kuwa mradi huo ,ulisanifiwa na kusimamiwa na mhandisi mshauri M/S Netwas (T) Ltd wa Dar es salaam mwaka 2009/2010 na Halmashauri na jamii ilishirikishwa katika hatua zote za kuibua mradi mpaka usanifu wake.

"Ujenzi ulianza mwaka wa fedha 2013/2014 chini ya mkandarasi M/S Federick company Ltd wa Dar es salaam kwa gharama ya sh.mil 359.577.570 "

Pia alibainisha kuwa ,kutokana na uhaba wa fedha kutoka serikali kuu ,mradi huu ulisimama kwa muda wa takriban miaka 2 mwaka 2015/2016 na kuendelea tena na ujenzi mwanzoni mwa mwaka 2017 na kukamilika mwezi agosti 2018.

"Mradi huo ulikuwa na vituo vya jamii vya kuchotea maji Tisa ambavyo vilikabidhiwa kwa uongozi wa watumia maji Muheza kwa ajili ya usimamizi.Hii iliweza kuongeza vituo viwili na kufanya jumla ya vituo vya jamii kuwa 11 na wateja binafsi 240 pamoja na kupeleka maji mtaa jirani wa Lumumba"

"Baada ya mradi kutanuka na maeneo mengine kupata huduma uongozi wa jumuiya ya watumiaji maji uliomba mradi ukabidhiwe DAWASA ili kusaidia huduma kuwa endelevu na kupunguza gharama za huduma ya maji"alifafanua Grace.

Mkongea aliukubali mradi huo na kusema maji ni haki ya kila mtu ,na aliiomba jamii kutunza vyanzo vyake ili miundombinu ya maji iweze kudumu.

Alisema, serikali inatekeleza kauli mbiu ya KUMTUA MAMA NDOO YA MAJI KICHWANI na kutekeleza sera ya maji ya mwaka 2002 ya kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kila upande kwa kila kaya pamoja na utunzaji wa vyanzo vya maji.

Awali mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama alisema ,mwenge wa Uhuru umepitia miradi 11 ,yenye thamani ya sh .bilioni 2.464.Assumpter alielezea, mradi mmoja umezinduliwa,mmoja umefunguliwa,miwili imewekwa mawe ya msingi na miradi saba imetembelewa

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RS Pwani Yaibuka Kidedea kwa Ushindi wa "-1 Dhidi ya Kibaha TC

    May 01, 2025
  • Rais Samia Apongezwa kwa kuwa Kiongozi wa Mfano katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mkoani Pwani

    May 01, 2025
  • RC Kunenge Aagiza CORECU Kutekeleza Maomo ya Rais Samia Kuhusub Ushirika

    April 30, 2025
  • Spika Tulia Asisitiza Umuhimu wa Muungano katika kuimarisha Umoja na Amani

    April 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.