• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

Pili Mnyema Aanza Rasmi Majukumu Kama Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani.

Posted on: June 27th, 2025

Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Pili Hassan Mnyema, amekabidhiwa rasmi ofisi leo Juni 27, 2025, kufuatia mabadiliko ya kiutendaji yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, mnamo Juni 23, 2025.

Katika mabadiliko hayo ya uongozi, Pili Mnyema amebadilishana vituo vya kazi na aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Rashid Mchatta, ambaye sasa atahudumu Mkoa wa Tanga.

Hafla ya makabidhiano imefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Kibaha.

Akizungumza baada ya kupokea ofisi, Mnyema alieleza kushukuru kwa kuendelea kuaminiwa na Mheshimiwa Rais, huku akiomba ushirikiano kutoka kwa watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Pwani.

“Ninaomba kwa dhati ushirikiano wenu. Sisi makatibu tawala ni waratibu tu, lakini utekelezaji wa shughuli za kila siku unafanywa na nyinyi. Kazi bila ushirikiano haiwezekani. Nipo tayari kuendelea kujifunza kutoka kwenu na pia kuwafundisha kwa yale niliyojifunza,” alisema Mnyema.

Kwa upande wake, Rashid Mchatta alitoa shukrani kwa uongozi wa mkoa na watumishi wote kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chake cha uongozi kilichodumu kwa miaka miwili na miezi mitatu.

“Nitumie fursa hii kuwashukuru kwa ushirikiano mkubwa mlionipa. Kwa uzoefu wangu, watumishi wa Mkoa wa Pwani mnajituma sana. Naomba muendelee kuonesha ushirikiano huo kwa Katibu Tawala mpya kama mlivyofanya kwangu,” alisema Mchatta.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa hafla hiyo, viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibaha, Regina Bieda; Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia, Shabani Shabani; Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kutoka Sekretarieti ya Mkoa, Obadia Malima; na Meneja wa TRA Mkoa wa Pwani, Masawe Masawe, waliwapongeza viongozi hao kwa kuaminiwa na Mheshimiwa Rais, huku wakiahidi ushirikiano wa karibu kwa Katibu Tawala mpya katika kutekeleza majukumu ya serikali kwa manufaa ya wananchi wa Mkoa wa Pwani.

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Pili Mnyema Aanza Rasmi Majukumu Kama Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani.

    June 27, 2025
  • Asasi za Kiraia Zatakiwa Kuimarisha Uwajibikaji, Uwazi na Ushirikiano na Serikali.

    June 26, 2025
  • RC Kunenge Aitaka Bodi ya Msaada wa Kisheria Kuongeza Elimu kwa Umma.

    June 24, 2025
  • RAS Pwani Afungua Mafunzo ya Mfumo wa PEPMIS kwa Watumishi wa Umma.

    June 20, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.