• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

Pwani yajipanga kufikisha asilimia 100 utoaji wa Chanjo ya UVIKO-19 ifikapo Diaemba 30 Mwaka huu

Posted on: November 23rd, 2022

MKoa wa Pwani umeandaa mpango wa kuwafikia wananchi nyumba kwa nyumba ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa kufikia lengo la asilimia 100 ya utoaji chanjo ya UVIKO-19 ifikapo Desemba 30 mwaka huu.

Lengo la mkakati huo ni kuongeza idadi ya watu waliochanja kwa kuwafikia wananchi popote walipo ili kufikia asilimia 100 kutoka asilimia 63 ya sasa.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Dk.Gunini Kamba alieleza hayo wakati wa kikao cha afya kilichofanyika Mjini Kibaha kikiwa na lengo la kujadili namna ya kufikia lengo la kitaifa la asilimia 100 katika utoaji wa chanjo hiyo.

Alieleza takwimu za chanjo ya UVIKO-19 hadi kufikia Novemba 22 wananchi 468,187 walikuwa tayari wamechanjwa sawa na asilimia 63 lengo likiwa ni kuwafikia walengwa 757,465.

Dk Gunini alisema mkakati huo utasaidia kuwafikia wazee ambao baadhi yao kutokana na umri wao kushindwa kwenda kwenye vituo vya afya pamoja na kundi la vijana ambalo mwamko wake umekuwa mdogo.

"Kutokana na kutofanya vizuri kulinganisha na mikoa iliyofanya vizuri , tumeona fursa iliyopo kufikia Lengo ni kupata usaidizi wa kiufundi na fedha kupitia mashirika mbalimbali ya kimataifa yanayojitokeza ikiwemo WHO na Agakhan foundation"alifafanua Gunini.

Mtaalamu wa chanjo kutoka Shirika la Afya duniani (WHO) Caroline Akim alieleza, takwimu za dunia wagonjwa wa UVIKO-19 ni miln 6.3, vifo 6.6 chanjo zilizotolewa ni biln 12.9 na kwa Afrika miln 9.3.

Alisema ,kwa upande wa Tanzania hadi kufikia Novemba 22 wagonjwa waliogundulika ni 38,205 vifo 845 kati ya hao 3,409 walikuwa watalaamu wa afya na kwamba chanjo milion 28.4 zimetolewa.

Akim aliongeza kuwa, mwishoni mwa wiki iliyopita wagonjwa wapya 105 waligundulika na Tanzania kwasasa imefikia asilimia 92 ya utoaji wa Chanjo ya UVIKO-19.

Nae Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Pwani Abbas Hincha alisema ,mkoa umefikia asilimia 63 ,na wilaya inayoongoza kwa jamii kujitokeza ni Kisarawe yenye asilimia 90,Kibiti asilimia 79 na Kibaha Vijijini asilimia 71.

Alielezea kwamba, changamoto zilizosababisha kutofikia malengo ya utoaji wa chanjo ,ni muitikio mdogo wa watoa huduma za afya katika uhamasishaji na uchanjaji kwenye baadhi ya maeneo.

Hincha alitaja changamoto nyingine ni uhaba wa radilimali fedha kwa ajili ya usambazaji wa chanjo na kliniki tembezi.

Waganga wakuu wa wilaya na wakuu wa wilaya ambazo hazijafanya vizuri walieleza wanaenda kuongeza nguvu ili kufikia malengo.

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RS Pwani Yaibuka Kidedea kwa Ushindi wa "-1 Dhidi ya Kibaha TC

    May 01, 2025
  • Rais Samia Apongezwa kwa kuwa Kiongozi wa Mfano katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mkoani Pwani

    May 01, 2025
  • RC Kunenge Aagiza CORECU Kutekeleza Maomo ya Rais Samia Kuhusub Ushirika

    April 30, 2025
  • Spika Tulia Asisitiza Umuhimu wa Muungano katika kuimarisha Umoja na Amani

    April 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.