Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, ambaye pia ni Skauti Mkuu wa Tanzania, Rashid Mchatta, amewahimiza watumishi wa Halmashauri ya Mafia kushirikiana, kujituma, na kutumia vipawa vyao katika kubuni mbinu mbalimbali za kuleta maendeleo wilayani humo.
Mchatta alitoa wito huoOtktoba 25 wakati alipofanya ziara fupi ya ukakaguzi katika Jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, ambalo ujenzi wake bado unaendelea.
Alisisitiza kuwa mshikamano na kujituma katika kazi, pamoja na matumizi ya vipawa vya kila mtu, ni muhimu katika kubuni na kutekeleza miradi ya kimaendeleo. “Tujitahidi kufanya kazi kwa kushirikiana na tutumie vipawa vyetu kubuni miradi ya kimaendeleo. Yale yanayofanyika Zanzibar, kwa nini tusiyafanye hapa?” alisema Bwana Mchatta.
Aidha, Mchatta alikagua pia ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kiegeani na kuagiza kuwekwa alama za mipaka (bikon) katika eneo la kituo hicho ili kuepuka migogoro ya ardhi hapo baadaye.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.