• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

RC Kunenge atatua changamoto za Stend ya Kibaha

Posted on: May 2nd, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge leo mei 2, 2023 ametembelea, kukagua, kusikiliza na kutatua kero za wasafiri kwenye Kituo cha Mabasi cha kibaha (Kibaha Bus Terminal).

Akiwa kwenye ukaguzi huo amesikiliza kero za Wananchi waliokuwa katika eneo hilo na kuzitatua huku akitoa maelekezo ya maboresho kutokanana na malalamiko ya wananchi kama yalivyofikishwa kwake.

Baadhi ya kero zilizowasilishwa kwake ni pamoja na kuchelewa kufika kwa mabasi ya Mwendekasi kituoni hapo ambayo yanafanya safari zake Kati ya Kibaha na Dar es Salaam, uduni wa mabanda ya kujikingia jua na mvua yaliyojengwa kwenye eneo hilo pamoja na kujaa maji kwa baadhi ya maeneo ya kituo hicho cha magari.

"Yaani tatizo lipo hapo hapo na tulipowaoneni tukasema leo kilio chetu kimekwisha, na ndio maana unaona nimekaa kule nikawafuateni fasta, yaani hicho ni kilio kikubwa saana," alisema Ashura Juma mkazi wa Kibaha, Picha ya ndege aliyekuwa kwenye kituo hicho cha magari.

Akitolea maelekezo ya utatuzi wa changamoto hizo, Mhe. Kunenge alisema kuwa kuhusu suala la magari ya mwendokasi atafuatilia kwa karibu kwa kiongozi msimamizi wa kampuni hiyo ingawa alipowasiliana  kwa simu na kuweka bayana kuwa wananchi wamelalamika kuwa kwa sasa huduma hiyo hairidhishi na kiongozi huyo kuahidi kuongeza Mabasi hayo na Viongozi wa DART kutembelea eneo hilo, pia alielekeza uongozi wa halmashauri ya Kibaha kufanya marekebisho kwenye mapungufu yaliyobainishwa kupitia hoja za wananchi (wasafiri) katika kituo hicho haraka iwezekanavyo.

Akijibu kero za Wananchi Kunenge alisema "nia ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake ni kutatua kero za Wananchi na kuwarahisishia utoaji wa Huduma."

Kuhusu eneo la kuegesha magari kuharibika na kujaa maji mabonde kwenye Kituo hicho ameagiza wataalam wa Halmshauri kushirikiana na TANROADS na TARURA kufanya matengenezo ya maeneo yaliyoharibika na akamtaka Mkurugenzi wa Mji kuangalia kuelekeza wataalam wake kufungua lango la kutokea abiria na kurekebisha mabanda ya abiria (vikingia mvua na jua) na kufanya maboresho.

Awali, Mhe. Kunenge alikagua na kuridhishwa na ujenzi wa barabara ya viuatilifu.

Pia alitembelea na kukagua maendeo ya ujenzi wa Kongani ya KAMAKA ambayo tayari uzio wenye urefu wa kilomita tisa, barabara za ndani, kituo cha zimamoto na cha Polisi vyenye thamani ya sh. Bilioni 23.3 vimekamilika.

Ziara hiyo ya Mhe. Kunenge ni sehemu ya mpango wake wa kuadhimisha miaka 59 ya Muungano kwa kukagua miradi kwa kila halmashauri katika Mkoa huo.

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RS Pwani Yaibuka Kidedea kwa Ushindi wa "-1 Dhidi ya Kibaha TC

    May 01, 2025
  • Rais Samia Apongezwa kwa kuwa Kiongozi wa Mfano katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mkoani Pwani

    May 01, 2025
  • RC Kunenge Aagiza CORECU Kutekeleza Maomo ya Rais Samia Kuhusub Ushirika

    April 30, 2025
  • Spika Tulia Asisitiza Umuhimu wa Muungano katika kuimarisha Umoja na Amani

    April 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.