Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amezihamasisha Mamlaka za Serikali za Mitaa mkoani humo kuongeza jitihada za kutumia fursa za kimaendeleo zilizopo ili kuboresha huduma na maisha ya jamii.
Kunenge ametoa hamasa hiyo kwa nyakati tofauti Juni 17, 2025 katika vikao vya Mabaraza Maalum ya Halmashauri za Wilaya ya Mkuranga na ya Kisarawe yanayojadili ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mwaka 2023/2024.
Ameeleza kuwa Mkoa huo unazo fursa lukuki ambazo zikifanyiwa kazi vizuri zinaweza kuufanya mkoa huo ukawa na mambo makubwa ya kimaendeleo yanayoweza kushangaza.
Akiwa Mkuranga, Kunenge aliwaeleza wajumbe wa Baraza la halmashauri la Wilaya hiyo kuwa wasikate tamaa katika harakati za kuwatafutia na kwapatia wananchi maendeleo kwa nguvu, akili na rasilimali walizonazo.
"Mimi siamini katika kushindwa na Dr. Samia Suluhu Hassan alisema haamini katika kushindwa ndiyo maana hata katika uandikishaji wapiga kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wetu uliongoza kwa kuwa jitihada zetu zinazingatia mtazamo wa kiamendeleo," alisema Kunenge.
Akiwa Kisarawe, mkuu huyo wa Mkoa alitumia fursa hiyo kuzipongeza halmashauri za mkoa wake kufanya vizuri katika kupunguza hoja zilizo ndani ya uwezo wao na sehemu kubwa ya zilizobaki ni za kisera ambazo zinategemea kuftqika iwapo zitatatuliwa na mamlaka zingine.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.