Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, amesema Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo (International Festival of Arts and Culture) lina mchango mkubwa katika kueneza ujumbe wa utamaduni duniani kote, kutangaza utalii wa Tanzania, na kudumisha ushirikiano wa kimataifa kutokana na ushiriki wa mataifa mbalimbali.
Kunenge aliyasema hayo katika siku ya tatu ya tamasha hilo, ambalo lilianza Oktoba 23. Aliwasihi Watanzania kuendelea kutangaza utalii wa nchi yao kwa bidii, akitolea mfano wa mafanikio ya filamu ya Royal Tour iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, aliwataka wasanii wa Bagamoyo kutumia tamasha hilo kama fursa ya kutoa elimu kwa jamii na kuimarisha uhusiano na wageni wanaotembelea Mji Mkongwe wa Bagamoyo, ili kukuza sekta ya utalii nchini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.