Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesisitiza umuhimu wa viongozi na watendaji kutoa taarifa za utelezaji miradi ya Serikali kwa kutoa takwimu ili kuonesha ufanisi wa utendaji wa Serikali ya awamu ya sita.
Kunenge ametoa msisitizo huo leo Julai 3, 2025 wakati akiongea na viongozi mbalimbali wa Mikoa ya Kanda ya Mashariki kwenye kikao cha maandalizi ya nanenane Kanda hiyo kilichofanyoka kwenye ukumbi wa Jeshi la Kujenga Taifa - JKT, viwanja Julius Kambarage Nyerere Mjini Morgoro.
"Maonesho ya mwaka huu ni ya kipekee kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa hela nyingi ambazo zimewezesha utekelezaji wa miradi mingi ikiwemo ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na utoaji huduma, hivyo mnapaswa kuyasemea kwa takwimu kuonesha ufanisi bila uoga" alisema Kunenge.
Maonesho ya Nanenane ni jukwaa muhimu la kuonesha mafanikio ya sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Biashara hivyo yanatoa fursa kwa wadau mbalimbali wa sekta hizo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.