MUHTASARI WA ORODHA YA VIWANDA MKOA WA PWANI NI KAMA IFUATAVYO:-
Jumla ya viwanda 1,535, vikiwemo viwanda 122 vikubwa, 120 vya kati, 276 vidogo na 1,017 vidogo sana (micro). Katika kipindi cha sita cha uongozi, jumla ya viwanda 131 vimeanzishwa, ambapo kati ya hivyo, viwanda 78 ni vikubwa.
Mkoa una jumla ya viwanda 119 vinavyojihusisha na uchakataji wa mazao ya kilimo na mifugo, hali inayowapa wananchi fursa kubwa ya kushiriki katika kukuza uchumi wa taifa.
Mkoa una viwanda vikubwa na vya kati vya kipekee ambavyo ni pamoja na:
• Viwanda 34 vya uchakataji wa mazao ya kilimo, kama vile:
Bagamoyo Sugar Ltd, Tanchoice, Tanlapia Ltd, Fuzzy International Co. Ltd, Unify Trading Corporation, Tera Cashew Processing Co. (T) Ltd.
• Viwanda 11 vya uzalishaji wa bidhaa za chakula, kama vile:
Bakhresa Food Products, Hill Packaging Co. Ltd, Sayona Fruit Products na U Fresh Co. Ltd.
• Viwanda 71 vya uzalishaji wa vifaa vya ujenzi, kama vile:
Twyford Ceramic Tiles, Hong Yu Steel, Kiluwa Steel and Allied Company, Surphier Float Glass Ltd, Lake Steel and Allied Company, Lodhia Steel Co. Ltd, Goodwill Ceramic Tanzania Ltd na BNBM Building Materials Co. Ltd.
• Viwanda 11 vya dawa za binadamu na mifugo, kama vile:
Kairuki International Co. Ltd, Hester Co. Ltd, Action Madero International Health Care na Bahari Pharmacy Co. Ltd.
• Viwanda 14 vya uzalishaji wa vifaa vya kufungashia, kama vile:
Hill Packaging Co. Ltd, TC Industries na Global Packaging.
• Viwanda 7 vya kuunganisha magari na pikipiki, kama vile:
GFA Assembling Co. Ltd, King Lion, Tata Africa Holding Tz, Motor Hub EA na Equar Suma JKT Ltd Vehicle Assembly Factory.
• Viwanda 17 vya uzalishaji wa vifaa vya umeme.
• Viwanda 12 vya uzalishaji wa bidhaa za plastiki.
• Viwanda vingine 32 ambavyo ni pamoja na:
King Lion Co. Ltd, KEDS Ltd, Hunan Power Group, Lake Steel Group Co. Ltd, Raddy Fibre Manufacturing Tz. Ltd, Instan Blue Industries Ltd na Fesho Group of Companies.
Kuangalia kiambatanisho A, Bofya Hapa
For more details about Investments Opportunities in Coast Region Click Here to Download.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.