SEKTA YA KILIMO
Eneo la Kilimo
Mkoa wa Pwani una eneo la takribani hekta 1,933,224 zinazofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali ambapo kwa sasa hekta 797,942 zinatumika sawa na 41.3% kwa shughuli za kilimo. Mazao makuu ya chakula yanayolimwa ni Muhogo, Mpunga, Mahindi, Viazi vitamu, Mbaazi, Mtama na jamii ya Mikunde. Mazao ya biashara ni Korosho, Nazi, Ufuta, Mbaazi, Pamba, Ndizi na Matunda (Machungwa, Mananasi, Maembe, na Makakala ‘Passion’).
4.2 Mazao ya chakula
Uzalishaji wa mazao ya chakula umekuwa ukiongezeka kutokana na usalma wa chakula umeendelea kuimarika kutokana na uzalishaji kuongezeka na elimu ya uhifadhi kutolewa kwa kaya. Katika msimu wa 2021/22 jumla ya tani 845,548.5, 2022/23 tani 985,881.7, 2023/2024 tani 1,244,835 na mwaka 2024/2025 jumla ya tani 1,765,897.87 za mazao ya chakula zilizalishwa. Hali ya chakula kwa mkoa ni toshelevu, vyakula vinapatikana kwa wingi katika maduka na soko kwa bei za kawaida.
4.3 Mazao ya Biashara
Mkoa wa Pwani ni miongozi mwa Mikoa inayozalisha mazao ya Biashara ambayo ni Korosho, Ufuta na Mbaazi ambapo mazao hayo huuzwa kupitia Mfumo wa Stakabadhi za ghala kupitia Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) ambapo wakulima, wanunuzi na wadau mbalimbali hupata fursa ya kufuatilia minada hiyo moja kwa moja kupitia simu janja au kompyuta.
Hali ya mauzo ya mazao ya Korosho, Ufuta na mbaazi kwa Mkoa wa Pwani imekuwa ikiongezeka ambapo kwa msimu wa 2025/2026 kiasi cha kilo 21,710,353 ziliuzwa zenye thamani ya shilingi 73,647,233,234.32, kilo 27,475,078 za ufuta zenye thamani ya shilingi 75,108,787,761.47 na kilo 298,655 za mbaazi zenye thamani ya shilingi 578,448,801.22.
4.5 Kilimo cha Umwagiliaji
Mkoa wa Pwani una eneo la hekta takribani 128,795 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Mkoa wa Pwani una jumla ya Miradi 16 ya umwagiliaji inayoendelea katika hatua mbalimbali katika Wilaya 6. Miradi minne (4) ya Ujenzi wa Mabwawa ipo katika Wilaya za Kibiti na Rufiji ambayo inahusisha Mabwawa 2 na skimu 2 zenye jumla ya Hekta 9,000. Skimu ya Ngorongo ambayo ipo Rufiji ina Hekta 3,000 na Skimu ya MBAKIAMTURI ambayo ipo Kibiti ina Hekta 6,000.
Miradi miwili (2) ya Ukarabati ipo katika Halmashauri ya Bagamoyo na Halmashauri ya Chalinze. Skimu ya CHAURU yenye jumla ya Hekta 720 ipo Halmashauri ya Chalinze na Skimu ya BIDP (Bagamoyo Irrigation Development Program) yenye Hekta 72 ipo Halmashauri ya Bagamoyo.
Aidha Miradi sita (7) ya Upembuzi yakinifu na Usanifu (Feasibility Study and Detailed Design) kwa ajili ya Mabwawa ya Umwagiliaji inaendelea na Mkandarasi yupo Site katika Wilaya tatu za Mkuranga, Kisarawe na Bagamoyo. Mkuranga ina mabwawa matatu ya Kitomondo, Kisere na Mbezi. Kisarawe ina mabwawa mawili ya Bwama na Mianzi na Bagamoyo kuna Bwawa moja la Mkoko. Halmashauri ya Kibaha Wilaya ujenzi wa Bwawa na skimu ya Mongomole ambapo ipo harua ya usanifu na upembuzi yakinifu.
Mkoa wa Pwani kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imepima jumla ya hekta 64,800 kwa ajili ay ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika bonde la Mto rufiji.
Huduma za Ugani
Mkoa wa Pwani kupitia Wizara ya Kilimo unaendelea kuimarisha huduma za ugani kwa kutoa vitendea kazi pamoja na huduma mbalimbali kama ifuatavyo:-
Mkoa kupitia Wizara ya Kilimo umepokea jumla ya pikipiki 324, vishikwambi 345 na vipima afya ya udongo 6 kwa ajili ya Maafisa ugani. Lengo la ugawaji wa vitendea kazi hivyo ni kuhakikisha Maafisa Ugani wanawafikia wakulima kwa urahisi ili kutoa elimu kwa ufanisi uliokusudiwa.
Wizara ya Kilimo imewezesha kujega nyumba 2 za Maafisa Ugani katika Halmashauri ya Kibaha (1) na Bagamoyo (1).
Wizara ya kilimo kupitia program ya Jenga kesho iliyo bora (BBT) imetoa Matrekta 6 (Halmashauri ya Kibaha -3 na Halmashauri ya Kisarawe- 3).
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.