Hali ya Upatikanaji wa Maji Mkoa wa Pwani.
Vyanzo vikuu vya maji katika Mkoa wa Pwani ni pamoja na mito mitatu (3) ya kudumu ya Rufiji, Ruvu na Wami, mabwawa ya asili na yale ya kutengenezwa na binadamu, uvunaji wa maji ya mvua na uchimbaji wa maji ya chini ya ardhi. Kulingana na sensa ya mwaka 2012 inaonyesha kwamba Mkoa wa Pwani ulikuwa na watu wapatao 1,098,668 na hadi kufikia mwezi Septemba, 2015, Mkoa ulikuwa ukitoa maji safi na salama kwa wakazi 834, 345 sawa na asilimia 75.9 ikilinganishwa na asilimia 60 ya mwaka 2005.
Upatikanaji huu wa maji unapishana kati ya Mijini na Vijijini. Takwimu zinaonyesha kwamba wakazi wa Vijijini wanaopata maji ni asilimia 75.5 ya wakazi wote wanaoishi Vijijini wakati asilimia 51.9 tu ya wakazi wanaoishi katika Makao Makuu ya Halmashauri za Miji ya Mkoa wa Pwani ndio wanaopata maji safi na salama. Hii ni pamoja na Miji ya Kibaha na Bagamoyo inayohudumiwa na mtandao wa mfumo wa maji wa DAWASA
Mamlaka za Bodi za Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Mkoa wa Pwani una Mamlaka za Maji sita (6). Mamlaka hizi nipamoja na DAWASA (ambayo inatoa huduma ya majisafi na ukusanyaji wa maji taka katika jiji la Dar es Salaam na Miji ya Kibaha na Bagamoyo), CHALIWASA (CHALINZE), Mamlaka za Maji za Miji ya Kilindoni (Mafia), Kisarawe, Mkuranga na Mamlaka ya Maji ya Mji wa Utete (Rufiji). Ukiiacha mamlaka ya maji ya DAWASA iliyopo katika daraja la A mamlaka tano zilizobaki zipo katika kundi la daraja C. (Picha hii ni mtambo wa kusafisha maji CHALIWASA).
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.