SEHEMU YA UFUATILIAJI WA MENEJIMENTI NA UKAGUZI
Kutoa usaidizi, utaalamu na huduma katika Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Sehemu hii itafanya shughulizifuatazo:
a) Kusimamia, kufuatilia na kutathmini uzingatiaji wa Sera, Sheria na Kanuni za Serikali katika Halmashauri;
b) Kukusanya, kuchambua na kuhakiki taarifa za fedha kutoka Halmashauri;
c) Kufanya Ufuatiliaji wa Fedha, Upimaji wa kazi za Ufuatiliajii na Tathmini (M&E) katika Halmashauri;
d) Kufuatilia Utekelezaji wa Mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika Halmashauri;
e) Kufuatilia na kupitia Mikataba ya Ufanisi wa kazi ya Halmashauri;
f) Kushauri na kujenga uwezo juu ya Usimamizi na Matumizi sahihi ya fedha za Umma katika Halmashauri;
g) Kusimamia na kukuza/kuboresha Mipango ya Uimarishaji wa mapato ya Halmashauri na kufuatilia utekelezaji wake;
h) Kukagua utendaji kazi wa Menejimenti katika Halmashauri;
i) Kuzitambua mbinu bora kutoka kwenye Halmashauri zinazofanya vizuri zaidi na kuziboresha zifae kutumiwa na Halmashauri zingine zinazofanana na hizo ndani ya Mkoa;
j) Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa kazi zilizoidhinishwa kwenye Muundo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa; na
k) Kufuatilia na kutathmini Ufanisi wa vikao vya kisheria vya Halmashauri na uzingatiaji wa Utawala Bora.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.