HUDUMA ZA AFYA MKOA WA PWANI
Sekta ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe inasimamiwa na timu ya usimamizi wa huduma za Afya Mkoa ‘Regional Health Management Team’(RHMT), ambaye mwenyekiti wake ni Katibu Tawala Msaidizi,sehemu ya Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii.
Timu hii hutoa ushauri wa kiufundi na kitaalam kwa Halmashauri na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa juu ya namna ya kuboresha huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kwenye maeneo yao. Kazi hii hufanyika kupitia usimamizi shirikishi kila robo mwaka na kila wakati kadri inavyohitajika kwa mujibu wa ratiba na miongozo ya Wizara ya Afya na OR-TAMISEMI. Usimamizi shirikishi huo unafanyika kupitia mfumo wa kielektroniki (AfyaSS). Katika kipindi cha Januari hadi Disemba 2024 jumla ya simamizi shirikishi 1,060 zilifanyika ngazi ya vituo na Halmashauri. RHMT kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Afya pia, inaratibu utoaji wa mafunzo mbalimbali kwa watoa huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe ili kuboresha huduma kwa wananchi.
Mkoa wa Pwani una vituo 590 vinavyotoa huduma za Afya yaani Hospitali 14, Vituo vya Afya 53, Zahanati 413, Maternity homes 07, Kliniki 18, na Maabara Binafsi 85. Hali ya umiliki wa vituo ni kama ifuatavyo, vituo 349 ni vya Serikali, 17 za taasisi za Serikali (Parastatal: yaani vituo vya Polisi, Magereza na Jeshi), 37 ni vya Mashirika ya Dini (Faith Based Organizations-FBO) na 77 ni vya Binafsi na 85 ni Maabara zinazojitegemea na kumilikiwa na Taasisi Binafsi.
Mchanganuo wa Idadi ya Vituo vya Kutolea Huduma za Afya 2025
Halmashauri
|
Hospitali |
Vituo vya Afya
|
Zahanati
|
Maternity Home
|
Kliniki
|
Maabara Binafsi
|
Jumla
|
Bagamoyo DC
|
2 |
7 |
27 |
2 |
5 |
13 |
56 |
Chalinze DC
|
1 |
8 |
72 |
1 |
0 |
19 |
101 |
Kibaha DC
|
1 |
6 |
37 |
0 |
1 |
10 |
55 |
Kibaha TC
|
4 |
8 |
40 |
0 |
9 |
22 |
83 |
Kibiti DC
|
2 |
5 |
68 |
0 |
0 |
2 |
77 |
Kisarawe DC
|
1 |
5 |
42 |
0 |
1 |
4 |
53 |
Mafia DC
|
1 |
2 |
24 |
0 |
0 |
2 |
29 |
Mkuranga DC
|
1 |
8 |
71 |
4 |
2 |
13 |
99 |
Rufiji DC
|
1 |
4 |
32 |
0 |
0 |
0 |
37 |
Jumla
|
14 |
53 |
413 |
7 |
18 |
85 |
590 |
Chanzo: Mfumo wa Usajili Vituo Wizara ya Afya (www.hfrs.moh.go.tz)-Februari 2025
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa - Tumbi ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Pwani tangu mwezi Julai mwaka 2011. Hospitali ina vitanda 210 na ina wafanyakazi 466. Hospitali inatoa huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD) wapatao 554 nawa ndani (IPD) 123 kwa siku na hutoa huduma kwa wakazi wa Pwani na Mikoa Jirani inayoizunguka (Dar es Salaam, Morogoro, Tanga n.k). Hospitali inatoa huduma za matibabu ya Kibingwa na Ubingwa Bobezi katika maeneo yafuatayo huduma za Magonjwa ya ndani, Magonjwa ya nje, huduma za Uraibu, Uchujaji wa damu (Dialysis), Magonjwa ya Dharura, Radiolojia, Uchunguzi wa Magonjwa, huduma ya Mama Baba na Mtoto, Upasuaji, Kinywa na Meno, Utengamao, Dawa na Maji tiba.
Upatikanaji wa Wataalam wa Afya - Mkoa una jumla ya watumishi 3,197 huku wanaohitajika ni 7,462 hivyo kuna upungufu wa watumishi 4,265 sawa na asilimia 57.2%. Mkoa umeweka mikakati mbalimbali ya kuwabakiza kazini watumishi ikiwemo kutoa elimu ya awali ya mafunzo kazini pamoja na kuwaingiza kwenye mfumo wa mshahara pamoja na kulipa stahiki zao. Sambamba na mkakati huo, Mkoa unafanya msawazo wa watumishi wa Afya kulingana na mahitaji na utaalam wa eneo husika ili kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi wote kwa usawa, uharaka na unafuu.
Hali ya Utoaji wa Chanjo za Kawaida - Katika kukinga watoto wa Umri wa Chini ya Miaka mitano na magonjwa yanayozuilika kwa Chanjo, Mkoa umeendelea na utoaji wa chanjo kwa kundi hili pamoja na uhamasishaji wa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanakamilisha chanjo. Hadi kufikia Disemba 2024, jumla ya watoto 89,010 (103%) kati ya walengwa 86,602 walipatiwa chanjo ya Penta inayokinga magonjwa saba. Pia watoto 86,157 (99%) kati ya walengwa 86,602 walikamilisha chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa Surua na wasichana 77,800 (291%) kati ya walengwa 26,846 walikamilisha Chanjo ya kuzuia Saratani ya Shingo ya Mlango wa Kizazi.
Hali ya Lishe mwaka 2024/2025 - Utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa lishe kwa ngazi ya Mkoa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 hadi kufikia mwezi Disemba vimetekelezwa kwa ufanisi wa juu. Halmashauri zilipanga kutumia jumla ya Tsh. 234,972,055 na hadi kufikia 15 Januari, 2025 jumla ya Tsh. na 344,269,177 sawa na 146.5% ya fedha hizo ziliweza kutumika kutekeleza afua mbalimbali za Lishe zilizopangwa kutekelezwa. Huduma ya matibabu kwa watoto wenye utapiamlo mkali zinazotolewa kwa watoto wote walioibuliwa kwa asilimia 100, vidonge vya kuongeza wekundu wa damu kwa wajawazito vimetolewa kwa asilimia 96.9%. Huduma ya chakula shuleni imetolewa kwa asilimia 92.7%, ingawa kumekuwa na changamoto ya idadi ya wanafunzi wanaonufaika na huduma hiyo kuwa ndogo.
Huduma ya Damu Salama Katika Vituo vya Huduma - Mkoa una jumla ya vituo 46 (Hospitali 14 na vituo vya Afya 32) vinavyotoa huduma ya Damu Salama kwa wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu. Katika kipindi cha Januari hadi Disemba 2024 zilikusanywa damu mifuko 19,549 (asilimia 119% ya malengo) toka kwa wananchi na mifuko 15,995 ilitumika kwa wagonjwa mbalimbali waliokuwa na uhitaji wa kuongezewa damu ndani ya Mkoa huku zaidi ya chupa 1,000 zilikwenda kusaidia wahitaji wengine vituo jirani nje ya Mkoa.
Huduma za Uchunguzi wa Magonjwa Mbalimbali - Mkoa una jumla ya Maabara 334 (74 ndani ya vituo vya Serikali, 175 kwenye vituo Binafsi na 85 Maabara Binafsi) zinazofanya huduma za kichunguzi wa magonjwa mbalimbali ya binadamu. Kati ya hivyo, vituo 97 vina uwezo wa kupima Kifua Kikuu na Ukoma na vituo 13 vina machine ya Gene-xpert inayoweza kupima Kifua Kikuu kwa kutumia vinasaba. Kuna Maabara mbili zilizopata hisabati ya kimataifa ya upimaji ((Accredited by SADCAS) yaani Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tumbi na Hospitali ya Wilaya Mkuranga. Huduma za Radiolojia zinapatikana katika Halmashauri zote za Mkoa wa Pwani kutokana na uwepo wa mashine za X-ray, Utrasound na uwepo wa Mtaalam mwenye sifa stahiki ya kuendesha mashine hizo. Pia Mkoa una jumla ya vituo 33 (24 vya Serikali na 9 Binafsi) vinavyotoa huduma ya kinywa na meno.
Huduma za Ustawi wa Jamii - Mkoa una Mabaraza ya Wazee 468 huku Wazee 71,141 wametambuliwa na kupatiwa vitambulisho vya matibabu. Kuna jumla ya vituo 355 vya kulelea watoto wakati wa mchana vilivyosajiliwa.katika kipindi cha Oktoba hadi Disemba 2024. Jumla ya wananchi 123,503 walipatiwa misahama kwenye matibabu ya Afya huku gharama yake ikiwa ni sawa na shilingi za Kitanzania 468,292,723.
Huduma ya Magonjwa ya Dharura na Milipuko - Mkoa una timu imara ya kukabiliana na magonjwa ya milipuko (Ebola, Marburg, Mpox, Cholera, Uviko-19 n.k) kuanzia ngazi ya kituo, Halmashauri na Mkoa (Rapid Response Team ‘RRT’)
Huduma za Uzazi - Mkoa una jumla ya vituo 393 ambavyo mama anaweza kwenda kujifungua kwa njia ya kawaida na salama, na endapo itatokea changamoto ya kujifungua kwa njia ya kawaida, kuna vituo 48 vinavyotoa huduma ya kujifungua kwa njia ya Upasuaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.