HUDUMA ZA AFYA
Sekta ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe inaongozwa na Dr BENEDICTO MUTALEMWA NGAIZA (MD, Msc(M&E) yeye ni Katibu Tawala Msaidizi huduma za Afya Ustawi wa Jamii na Lishe na ni Mganga Mkuu wa Mkoa. Pia ni mwenyekiti wa timu ya usimamizi wa huduma za afya Mkoa ‘Regional Health Management Team’(RHMT)
Timu hii hutoa ushauri wa kiufundi na kitaalam kwa Halmashauri na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa juu ya namna ya kuboresha huduma za afya, ustawi wa jamii na lishe kwenye maeneo yao. Kazi hii hufanyika kwa kufanya usimamizi elekezi kila robo mwaka na kila wakati kadri inavyohitajika kwa mujibu wa ratiba. RHMT kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaratibu utoaji wa mafunzo mbalimbali kwa watoa huduma za afya, ustawi wa jamii na lishe ili kuboresha huduma kwa wananchi.
Mkoa wa Pwani una vituo 455 vinavyotoa huduma za afya ambapo vituo 12 ni Hospitali, 48 ni Vituo vya Afya, 373 ni Zahanati, 16 ni Kliniki na 6 ni “Maternity home”. Hali ya umiliki ni vituo 333 ni vya Serikali, 37 ni vya Mashirika ya Dini na 85 ni vya binafsi.
Mchanganuo wa Idadi ya Vituo vya kutolea huduma za Afya
Na. |
Halmashauri |
Hospitali |
Vituo vya Afya |
Zahanati |
Kliniki |
Maternity |
Jumla |
1 |
Bagamoyo
|
1 |
4 |
26 |
4 |
2 |
37 |
2 |
Chalinze
|
1 |
8 |
62 |
0 |
1 |
72 |
3 |
Kibaha Wilaya
|
1 |
5 |
35 |
1 |
0 |
42 |
4 |
Kibaha Mji
|
3 |
8 |
40 |
9 |
0 |
60 |
5 |
Kibiti
|
2 |
5 |
66 |
0 |
0 |
73 |
6 |
Kisarawe
|
1 |
5 |
40 |
1 |
0 |
47 |
7 |
Mafia
|
1 |
1 |
22 |
0 |
0 |
24 |
8 |
Mkuranga
|
1 |
8 |
54 |
1 |
3 |
67 |
9 |
Rufiji
|
1 |
4 |
28 |
0 |
0 |
33 |
Jumla |
12 |
48 |
373 |
16 |
6 |
455 |
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Hospitali ya Mkoa ya Rufaa Tumbi ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Pwani tangu mwezi Julai mwaka 2011. Hospitali ina vitanda 281 na ina wafanyakazi 508. Hospitali hutoa huduma kwa wagonjwa wapatao 500 kwa siku na hutoa huduma kwa wakazi kutoka Dar es Salaam. Hospitali inatoa huduma za matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi katika maeneo yafuatayo huduma za magonjwa ya ndani, magonjwa ya nje, huduma za uraibu, huduma za uchujaji wa damu (Dialysis), huduma za magonjwa ya dharura, huduma za radiologia, huduma za uchunguzi wa magonjwa, huduma za mama baba na mtoto, huduma za upasuaji, huduma za kinywa na meno, huduma za utengamao, huduma za madawa na maji tiba.
Upatikanaji wa Wataalam wa Afya. Mkoa una jumla ya Watumishi 3,306 dhidi ya wanaohitajika 6,398 hivyo kuna upungufu wa watumishi 3,092 sawa na asilimia 48. Mkoa umeweka mikakati mbalimbali ya kuwabakiza kazini watumishi ikiwemo kutoa elimu ya awali ya mafunzo kazini pamoja na kuwaingiza kwenye mfumo wa mshahara pamoja na kulipa stahiki zao. Sambamba na mkkati huu mkoa unafanya msawazo wa watumishi wa afya kulingana na mahitaji na utaalam wao ili kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi wote kwa usawa na unafuu.
Utoaji wa Chanjo ya UVIKO-19 na Chanjo za Kawaida
Katika kupambana na ugonjwa wa UVIKO - 19, Mkoa umeendelea kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ikiwa ni sambamba na kuhamasisha Wananchi kupata chanjo. Hadi kufikia, Disemba 2023 Mkoa umepokea jumla ya Dozi 1,015,965 za chanjo ambapo watu 923,825 kati ya walengwa wa mkoa 757,465 wamepata chanjo sawa na asilimia 122.Vile vile Mkoa umeanza kutoa Dozi ya nyongeza ya UVIKO-19 “ Booster Doze “ ambapo hadi Disemba 2023 watu 62,495 kati ya walengwa 63,000 wamepata chanjo sawa na asilimia 99.1.
Katika Kukinga watoto wa Umri wa Chini ya Miaka mitano na magonjwa yanayozuilika kwa Chanjo, Mkoa umeendelea na utoaji wa chanjo kwa kundi hili pamoja na uhamasishaji wa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanakamilisha chanjo. Hadi kufikia Disemba 2023 Jumla ya watoto 69,950 walipatiwa chanjo ya Penta inayokinga magonjwa saba sawa na asilimia 165.
Pia watoto 74,385 (176%) walikamilisha chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa Surua na Wasichana 21,567 (144%) walikamilisha Chanjo ya kuzuia Saratani ya Shingo ya Mlango wa Kizazi.
Hali ya Lishe mwaka 2022/2023
Utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa lishe kwa ngazi ya Mkoa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 hadi kufikia mwezi Disemba vimetekelezwa kwa ufanisi wa juu. Mwenendo wa utekelezaji wa Mkataba wa Lishe ngazi ya Halmashauri ni wa ufanisi wa juu katika viashiria vingi ikiwepo kiashiria cha Utoaji wa elimu ya Lishe ngazi ya jamii na katika vituo vya kutolea huduma za afya (100%). Vilevile, kiashiria cha utoaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa afua za Lishe kimetekelezwa kwa ufanisi ambapo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai-Disemba, 2023 Halmashauri zilipanga kutumia jumla ya Tsh. 315,469,107 na mpaka kufikia tarehe 31 Disemba, 2023 jumla ya Tsh. 271,506,492 sawa na 86% zilitumika kutekeleza afua za Lishe.
Mkoa umeendelea kuimarisha uratibu na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za lishe ambazo baadhi yake ni pamoja na;-
Huduma ya matibabu kwa watoto wenye utapiamlo mkali zinazotolewa kwa watoto wote walioibuliwa kwa asilimia 100, vidonge vya kuongeza wekundu wa damu kwa wajawazito vimetolewa kwa asilimia 96.9; siku za afya na lishe ya mtoto za kijiji/mitaa zimetekelezwa kwa asilimia 96.7,
Huduma ya chakula shuleni imetolewa kwa asilimia 99.3, ingawa kumekuwa na changamoto ya idadi ya wanafunzi wanaonufaika na huduma hiyo kuwa ndogo.
Vikao vya tathmini ya mkataba wa lishe ngazi ya Mkoa vimefanyika kama inavyoelekezwa (100%) na taarifa kuwasilishwa OR – TAMISEMI kwa wakati. Kwa ngazi ya Halmashauri, vikao vya tathmini vimetekelezwa pia kwa asilimia 100.
Huduma za Lishe kwa magonjwa yasiyoambukiza (Kisukari, saratani, shinikizo la juu la damu, magonjwa ya figo n.k) na msaada wa kitaalamu umetolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa-Tumbi na Hospitali zote za Wilaya kwa wagonjwa wa nje na waliolazwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.