Sekta hii inaongozwa na Afisa Elimu Mkoa kwa kushirikiana na wasaidizi wake ambao ni Maafisa Elimu Taaluma, Afisa Elimu Watu Wazima, Afisa Michezo, na Afisa Utamaduni. Mkoa una jumla ya Shule za Msingi 837 kati ya shule hizo 652 ni za Serikali na 185 zinamilikiwa na Watu binafsi na Mashirika ya Dini. Shule hizo zina jumla ya wanafunzi 441,981 kuanzia darasa la Awali hadi darasa la saba wakiwemo wavulana 220,094 na wasichana 221,887.
Shule za Sekondari zilizopo ni 291 kati ya hizo shule 193 ni za Serikali na 98 ni za binafsi. Idadi ya wanafunzi kuanzia Kidato cha I – VI ni 166,308 wakiwemo wavulana 76,467 na wasichana ni 89,841.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
79
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
106
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Mkoa unatekeleza Mpango wa Utoaji wa Huduma ya Chakula Shuleni ili kuhakikisha Shule zote za Msingi na Sekondari zinatoa chakula kwa wanafunzi ambapo uzinduzi wa Mpango wa Utoaji wa Huduma ya Chakula Shuleni umefanyika katika Ngazi ya Mkoa, Halmashauri, Kata na Shule/Kijiji/Mtaa. Jumla ya wanafunzi 316,899 kati ya 441,981 wa shule za Msingi sawa na asilimia 71.70 wanapata chakula wakiwa shule na Wanafunzi 85,903 kati ya 166,308 wa shule za sekondari sawa na asilimia 51.65 wanapata chakula wakiwa shule. Aina ya chakula wanachopatiwa ni pamoja na ugali, wali, uji, kande, nyama, maharage, mboga za majani, mihogo na viazi.
Mkoa katika mwaka 2022/23 umepokea Shilingi 5,857,771,698.47 kwa ajili ya ujenzi viwili vya Ufundi Stadi (VETA) katika Halmashauri ya Mafia Shilingi 3,164,227,684.47 na Shilingi 2,693,544,014.00 katika Halmashauri ya Rufiji. Aidha mwaka 2023/24 Serikali imetoa Shilingi 1,388,970,608.03 kwa ajili ya ujenzi wa vyuo vya ufundi (VETA) vinne (4) katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Mkuranga, Chalinze na Kisarawe.
Mkoa umeteua Shule ya Sekondari Kibaha kuwa kiungo cha Shule za Sekondari katika ufundishaji mubashara (Live Teaching) kwa kuwa vifaa vya ufundishaji vimefungwa katika shule hiyo. Ufundishaji wa darasa janja utasaidia kukabiliana na changamoto ya upungufu wa walimu hususani katika masomo ya Hisabati na Sayansi, kukatisha masomo kutokana na kufungwa shule kunakosababishwa na mlipuko wa magonjwa na majanga mengine. Aidha, Mkoa umepokea kiasi cha shilingi 1,510,884,242.85 kwa ajili ya utekelezaji wa afua za program ya Shule Bora hususani mafunzo kwa walimu.
Katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali imegharamia Elimu msingi bila malipo katika maeneo ya ruzuku ya Uendeshaji wa shule (Capitation), chakula, fidia ya ada ya wanafunzi na posho ya madaraka kwa walimu wakuu, wakuu wa shule na Maafisa elimu Kata. Katika mwaka wa fedha 2024/2025 hadi kufikia mwezi Juni, 2025 jumla ya shilingi 17,557,395,959.00 zimepokelewa.
Mwaka 2024/2025 Mkoa umepokea Shilingi 23,230,366,360.70 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule za msingi na sekondari. Katika kiasi hicho shilingi 1,944,800,000 zimopokelewa kupitia mradi wa GPE TSP, shilingi 4,392,393.696 zimepokelewa kupitia mradi wa SEQUIP, shilingi 2,183,600,000 zimepokelewa kupitia programu ya EP4R, shilingi 3,626,579,977 zimepokelewa kutoka Serikali kuu, shilingi 14,853,708,241.00 zimepokelewa mradi wa BOOST, shilingi 280,000,000 zimepokelewa programu ya IPOSA,shilingi 289,685,749 zimepokelewa kutoka programu ya SRWSSP na shilingi 47,600,000 zimepokelewa programu ya LANES II.
Kupitia miradi mbalimbali Mkoa umekuwa ukipokea fedha kwa awamu kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, maabara, maktaba, bwalo, mabweni, majengo ya utawala pamoja na ukarabati.
Hata hivyo, Juhudi zaidi zinaendelea kufanyika ili kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya wanafunzi wanaopata daraja sifuri na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata daraja la kwanza hadi la tatu katika Mtihani wa Kidato cha Nne na Upimaji wa Kidato cha Pili.
Kidato cha sita ufaulu ni asilimia 99.85 kwa mwaka 2024 na kwa mwaka 2025 ufaulu ni asilimia 99.59 ambapo hakuna mwanafunzi aliyepata Divisheni 0.
Kidato cha nne kutoka asilimia 83.84 mwaka 2022 hadi asilimia 90.17 mwaka 2024 na
Kidato cha Pili Kutoka asilimia 79.93 mwaka 2022 hadi asilimia 83.14 ya mwaka 2024;
Darasa la Nne kutoka asilimia 88.14 ya mwaka 2022 hadi kufikia 89.06 ya mwaka 2024;
Mkoa umepata mafanikio makubwa sana katika ufaulu kama ifuatavyo;-
Mkoa una jumla ya Walimu 7,043 wa Shule za Msingi sawa na asilimia 70.91 ya mahitaji ya walimu 9,932 na Walimu 5,020 wa Shule za Sekondari sawa na asilimia 86.59 ya mahitaji ya walimu 5,797. Aidha, Serikali inaendelea kuajiri walimu ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa walimu. Mwaka 2021/22, 2022/23 na 2024/25 Mkoa umepokea walimu wa ajira mpya 1,187 ikiwa 446 wa shule za Msingi na 741 wa shule za Sekondari.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.