Mkoa unatekeleza Mradi wa ujenzi wa Bandari Kavu ya Kwala - Ruvu Wilaya ya Kibaha ambapo awamu ya kwanza na ya Pili ya ujenzi umekamilika. Shughuli zilizofanyika ni pamoja na ujenzi wa barabara ya lami km 15 kutoka vigwaza hadi eneo la Bandari kwala. Aidha, katika harakati za kuunganisha kisiwa cha Mafia, Serikali ilinunua Kivuko cha MV Kilindoni kilichogharimu Shilingi Bilioni 5.3. kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria mia mbili (200), magari Sita (6) kinafanya safari zake kati ya (Nyamisati - Mafia) hivyo kupunguza shida ya usafiri kwa wananchi wa Mafia. Mkoa umeendelea kutengewa fedha kila mwaka kwa ajili ya kivuko kingine kipya. Hadi mwezi Juni 2023 jumla ya Shilingi Bilioni 2 zimetengwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.