Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Dkt Delphine Magere amewataka watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia kufanya kazi kwa juhudi na malengo ili kuiletea Wilaya hiyo maendeleo.
Akizungumza na Watumishi wa halmashauri hiyo , Dkt Magere amesema kuwa uwajibikaji, Upendo na Mawasiliano ndio njia muhimu itakayoweza kuisaidia kuleta maendeleo Mafia
Amewataka kufuata taratibu ,Sheria na kanuni za utumishi wa umma katika shughuli zao za kila siku pamoja na kushirikiana katika masuala mbalimbali.
Hayo ameyasema leo wakati alipofanya kikao cha pamoja na watumishi walioko katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na wale wa halmashauri hiyo.
“Napenda kuwaambia kuwa tunapaswa kushirikiana katika kila jambo kwa maendeleo ya Mafia na kila mtu anapaswa kuwajibika katika nafasi yake kwa malengo ya kuifanya Mafia iwe Mpya” alisema Dkt Magere.
Aidha ameeleza kuwa kusuhu suala la uhaba wa watumishi katika wilaya hiyo Dr Magere amesema kuwa suala hilo atalichukua na kulifikisha mahala husika ili liweze kufanyiwa kazi kwa hatua Zaidi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.