Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhe. Abubakar Kunenge leo Agost 5 2024 ametembelea Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki yanayohusisha Mikoa ya Pwani, Morogoro Tanga na Dar es salaam.
Akiwa kwenye Viwanja hivyo Kungenge ametembelea mabanda ya Monesho na Vitalu mbalimbali vya mazao ya Kilimo na mifugo.
Pia Kunenge amepongeza Taasis za Utafiti kwa kufanya Tafit Nzuri na amewataka kushirikiana na Wakulima ili wajifunze kwa vitendo.
Amemshukuru Mhe Rais kwa utoaji wa Pembejeo na Viuatilifu.
Ameeleza kuwa Kanda hiyo ya Mashariki inakuwa kasi katika kilimo cha mazao ya biashara na Chakula na kuwa wana matunda na vyakula vingi ikiwemo mboga za Majani ambapo wakulima wanatumia teknolojia rahisi katika kuhifadi mazao hayo ili yasiharibike.
Katika hatua nyingine Kunenge ameendelea kuhimiza matumizi ya Nishati mbadala ambapo amewataka wadau wote wanaohusika na utengenenzaji wa nishati hizo kujitangaza zaidi na kushirikiana na shirika la STAMICO ili kupata masoko na kufikia Wannachi.
Aidha amewataka Watalaam kufanya tathimini ya maonesho haya ili kuendelea kuboresha maonesho hayo ili kwenda pamoja na maono ya Mhe Rais ikiwemo lile la kulisha Dunia.
Ameyataka pia Makampuni yaliyoshiriki maonesho hayo kutumia wanaufaika wa huduma na teknlojia zao kueleza mafanikio na tija walizopata na amewasisitiza wataalam hao kutoa mafanikio yenye tija yanayogusa wananchi na watu wa kawaida.
Wakati huo huo RC Kunenge amezitaka Halmshauri kuangali uwezekano wa kutoa mikopo ya Vijana wanawake na wenyewe ulemavu kwa vikundi kwa kutoa mikopo kwa ajili shughuli za utengenezaji wa nishati mbadala kwa kutumia mabaki ya miwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.