Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge leo Julai 21, 2022 amekabidhi matrekta 10 yenye thamani ya Sh. Milioni 700 kwa Kikundi cha Wakulima wa Mpunga kiitwacho MBAKIAMTURI kilichopo wilayani Kibiti.
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi matrekta hayo yenye Majembe yao kwenye viwanja vya Stendi ya Mabasi Kibiti, RC Kunenge Amewapongeza wanakikundi hao kwa kuwekeza katika kilimo Mkoani Pwani na akawaasa kuzingatia Umuhimu wa kilimo cha kitaalam kwa kutumia mitambo ya kisasa na kufuata kanuni za kilimo pia kutotegemea Mvua pekee bali walime kwa kutumia umwagiliaji huku akibainisha kuwa Atawasiliana na Waziri wa kilimo ili Ujenzi Miundombinu ya umwagiliaji ijengwe kwenye eneo la mradi huo.
“Umoja wenu ni nguvu yenu na kwa kupitia umoja huo mmeanza kunufaika kwa kupata zana za kilimo.” Alisema RC Kunenge.
Kuhusu Changamoto ya migogoro kati ya Wakulima na Wafugaji RC kunenge ameeleza kuwa linafanyiwa kazi Ipasavyo kwa kusimamia Matumizi bora ya Ardhi na akawataka Viongozi wa Wilaya hiyo kuwasaidia wakazi na Vijana kujiunga kwenye vikundi hivyo na kuboresha maisha.
Ameeleza kuwa Katika Mkoa wa Pwani zao la Mpunga linalimwa Rufiji (Nyamweke) Chalinze(CHAURU) Bagamoyo (BIDP) Kibaha Mongomole na Kibiti na kwamba mazao mengine ya kibiashara yanayolimwa Mkoani hapo ni pamoja na Katani, Ufuta Korosho, Miwa, Michikikichi, Mpunga, Nazi na mengine Mengi.
Ameongeza kuwa kwa msimu huu Jumla ya Tan 18,266 za ufuta zimeuzwa na kuingizia wakulima Bilioni 57.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.