Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Abubakari Kunenge ,amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato na kusimamia vizuri matumizi ya fedha ya miradi ya maendeleo.
Aidha amekiagiza kitengo cha TEHAMA (IT) kubuni mifumo iliyo bora ya ukusanyaji wa mapato kwa pamoja ili kuweza kuzuia mianya ya ubadhilifu.
Rai hiyo ameitoa leo Oktoba 27 wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kilicho wahusisha viongozi wa Mkoa ambao ni Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wenyeviti,Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Idara , Vitengo Sekretariet ya Mkoa pamoja na wakuu wa taasisi ya umma.
Amewataka watendaji wote kufanya kazi kwa weledi ili kuweza kufikia malengo ambayo mkoa umejiwekea.
Vilevile amewaasa viongozi wa mkoa kuwasimamia ipasavyo wasaidizi wao pamoja na kushirikiana ili kuleta maendeleo ya Mkoa.
Kunenge amesema, matarajio yake makubwa kuona mkoa unafanya vizuri katika sekta zote pamoja na kutatua kero zinazowakabili wananchi.
Mkuu huyo wa Mkoa ,amewataka Wakuu wa Taasisi za Umma kuhakikisha wanatatua changamoto zote zinazowakabili wananchi hasa katika sekta za Maji, Nishati ya umeme na barabara.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.