Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo ametoa muda wa mwezi mmoja kwa mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza marumaru cha KEDA kilichopo Pingo Chalinze Mkoa ni hapa kutekeleza ahadi zote alizoingia na serikali ya kijiji cha Pingo wakati alipofika katika kijiji hicho kuomba kuomba apatiwe ardhi kwa ajili ya kujenga kiwanda hicho.
Mhandisi Ndikilo ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wakazi wa kjiji hicho wakilalamikia uongozi wa kiwanda hicho kushindwa kutekeleza ahadi walizowaahidi kwamba aendapo wangewapatia ardhi wangewasaidia kuwajengea nyumba ya mwalimu katika kijiji hicho pamoja na kuwasaidia ukamilishaji wa ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya Pera lakini chakushangaza ahadi hizo hazijatakeleza kwa miaka mitatu .
Akizungumza kwa niaba ya wanakijiji hao mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amesema kuwa kutotetekelezwa kwa ahadi hizo kunaweza kukaibua chuki baiana ya wakazi wa kijiji hicho na mwekezaji jambo ambalo linaweza kuchafua taswira ya nchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa waPwani Mhandisi Ndikilo ameonyesha kusikitishwa kwake na mmiliki huyo kushindwa kutekeleza kwa wakati ahadi alizoingia na wananchi na hivyo kumpa muda wa siku thalathini awe amezitekeleza ahadi hiyo ya kumalizia Zahanati pamoja na Nyumba ya mwalimu.
“Nawapa mwezi Mmoja kutoka leo mkamilishe ahadi yenu mlioingia na serikali ya kijiji ambayo mliyoahidiana wakati mnakabidhiana ardhi, kwani ni aibu kwa kampuni kubwa kama hii ya KEDA kushindwa kutimiza ahadi waliyowekeana na sitaki nisikie tena suala hili ambalo niliulizwa mwaka jana na nikatoa maelekezo kwa Twayford na sasa KEDA wayamalizie leo wananchi wangu wanaendelea kufatilia hilo hapana jengeni uaminifu kati ya wawekezaji na wananchi ili muendelee kushirikiana”alisema Mhandisi Ndikilo
Aidha ametoa rai kwa wawekezaji wote wa Viwanda kurudisha faida kidogo kwa jamii inayoizunguka ili wananchi waweze kufaidika uwekezaji huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.