Watumishi katika halmashauri za mkoa wa Pwani wametakiwa kuacha kufanya siasa na kufanya kazi kwa weledi zaidi huku wakifuata kanuni na sheria za Serikali katika utendaji wa kazi zao.
Rai hiyo imetolewa na Katibu tawala mkoa wa Pwani , Ndugu Zuberi samataba wakati akifunga kikao maalum cha kupitia hoja za mkaguzi wa hesabu za Serikali ( CAG) mwanzoni mwa wiki hii wilayani Mafia.
“Ningependa sisi watalaam tufanye kazi zetu za kitaalam za kushauri kitalaam kulingana na taaluma zetu na kuandaa taarifa mbalimbali za kazi na siasa tuwaachie wenzetu wanasiasa ”alisema Samataba
Aidha ameipongeza Halmashauri ya ya Wilaya ya mafia kwa kuweza kupata hati safi na pia amesema amefarijika sana kuona Halmashauri zote za Mkoa wa Pwani zimepata hati safi.
Samataba amesema kuwa kupata hati safi si jambo dogo hivyo amezitaka Halmashauri kuwa makini katika kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za Serikali na amesisitiza kwamba katika mkoa wake hataki kuona hati chafu. Au yenye mashaka.
Naye Mkaguzi Mkuu wa Mkoa Pwani ndugu Eliudi Masombolwa amesema kuwa ukaguzi umefanywa kwa viwango vya kimataifa, lengo likiwa ni kuona kama kuna ubadhirifu umefanyika na sheria na kanuni za matumizi ya fedha za Serikali zimezingatiwa.
Aidha, alisema kupata hati safi hakuimanisha kwamba hakuna shida katika matumizi ya fedha za Serikali kwa asilimia mia moja(100%) isipokuwa Halmashauri imefanikiwa kudhibiti malengo mabaya yanayoweza kuathiri matumizi mazuri ya fedha za Serikali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.