SEKTA YA KILIMO
Mkoa wa Pwani una eneo la takribani hekta 1,933,224 zinazofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali ambapo kwa sasa hekta 797,942 zinatumika sawa na 41.3% kwa shughuli za kilimo.
Mkoa wa Pwani una eneo la hekta takribani 128,795 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Mkoa wa Pwani una jumla ya Miradi 16 ya umwagiliaji inayoendelea katika hatua mbalimbali katika Wilaya 6. Miradi minne (4) ya Ujenzi wa Mabwawa ipo katika Wilaya za Kibiti na Rufiji ambayo inahusisha Mabwawa 2 na skimu 2 zenye jumla ya Hekta 9,000. Skimu ya Ngorongo ambayo ipo Rufiji ina Hekta 3,000 na Skimu ya MBAKIAMTURI ambayo ipo Kibiti ina Hekta 6,000.
Miradi miwili (2) ya Ukarabati ipo katika Halmashauri ya Bagamoyo na Halmashauri ya Chalinze. Skimu ya CHAURU yenye jumla ya Hekta 720 ipo Halmashauri ya Chalinze na Skimu ya BIDP (Bagamoyo Irrigation Development Program) yenye Hekta 56 ipo Halmashauri ya Bagamoyo.
Aidha Miradi sita (6) ya Upembuzi yakinifu na Usanifu (Feasibility Study and Detailed Design) kwa ajili ya Mabwawa ya Umwagiliaji inaendelea na Mkandarasi yupo Site katika Wilaya tatu za Mkuranga, Kisarawe na Bagamoyo. Mkuranga ina mabwawa matatu ya Kitomondo, Kisere na Mbezi. Kisarawe ina mabwawa mawili ya Bwama na Mianzi na Bagamoyo kuna Bwawa moja la Mkoko.
Mkoa wa Pwani kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imepima jumla ya hekta 64,800 kwa ajili ay ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika bonde la Mto rufiji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.