SEKTA YA MIFUGO
Ufugaji ni moja ya shughuli za kiuchumi katika Mkoa wa Pwani hasa ufugaji wa ng'ombe wa asili. Ng’ombe wa maziwa walioboreshwa pia hufugwa katika Halmashauri zote hasa maeneo ya pembezoni mwa miji. Wanyama wengine wa kufugwa ambao wanasaidia maisha ya watu ni mbuzi, kondoo, punda, nguruwe na kuku.
Idadi ya Mifugo
Mkoa una jumla ya ng’ombe 697,323 (kienyeji 654,942, maziwa 34,508 na nyama 7,873), mbuzi 273,292, kondoo 122,876, nguruwe 26,895, punda 3,524 na kuku 3,187,092 (asili 1,220,069, nyama 1,132,796 and mayai 834,232). Chalinze ndiyo yenye idadi kubwa ya ng’ombe (258,370) ikifuatiwa na Kisarawe (87,827), Rufiji (83,197), Kibaha (73,996), Kibiti (68,294), Bagamoyo (44,415), Mkuranga (37,515), Mafia (13,301 Halmashauri ya Mji wa Kibaha) (7) na Kibaha (7)
Chalinze pia ina idadi kubwa ya mbuzi (155,639) ikifuatiwa na Kisarawe (33,698), Kibaha (21,393), Rufiji (16,765), Kibiti (16,062), Mkuranga (12,990), Bagamoyo (10,518), Kibaha Mjini (5,229) na Mafia (5,229). Idadi kubwa ya kondoo wanapatikana Chalinze (65,340), ikifuatiwa na Bagamoyo (17,430), Kisarawe (12,092), Kibaha (11,218), Rufiji (6,175), Kibiti (4,327), Mkuranga (4,157), Kibaha Mjini (838) na Mafia (98). Kuku wanaishi sana Kisarawe (682,297) wakifuatiwa na Bagamoyo (609,039), Kibaha Mjini (532,526), Kibaha (427,341), Mkuranga (296,555), Chalinze (266,336), Kibiti (238,361), Rufiji (207,071), Rufiji (238,361), Rufiji (207) 207.
Mazao ya Mifugo
Mazao mbalimbali yanayotokana na mifugo ni pamoja na mziwa lita 21,023,471, nyama kilo 7,526, mayai trei 2,617,457, ngozi za ng’ombe vipande 789,282 na ngozi za mbuzi na kondoo vipande 21,610.
Miundombinu ya Mifugo
Miundombinu ya mifugo iliyopo ni minada 28, machinjio ya kisasa 3, machinjio ndogo 7, makaro 29 na majosho 70 yanayofanya kazi.
Afua za kukabiliana na Ufugaji wa Kuhamahama
Mkoa una tekeleza mpango wa ranchi ndogo kwa kushirikiana na Chama cha Wafugaji Tanzania Mkoa wa Pwani. Lengo ni kuwezesha wafugaji kumiliki maeneo ya malisho na kuyaendeleza kwa kujenga miundombinu na kupanda malisho bora. Hadi kufikia Julai 2025, jumla ya vitalu (ranchi ndogo) 528 vyenye eneo la hekta 29,454 vimepimwa na kugawiwa jumla ya wafugaji 620 wenye mifugo 70,973 katika Wilaya za Chalinze, Kibiti, Kisarawe na Rufiji. Wafugaji 136 wamepatiwa hati miliki katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.