Taasisi ya kifedha ya Bank ya Stanbic ,imekabidhi vyumba vya madarasa Kumi na kuahidi kutoa madawati 100 kwa taasisi ya Watoto Wetu Tanzania, inayojihusisha na kutoa elimu kwa watoto wenye Mazingira magumu na hatarishi huko Mazizi ,Msata Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Stanbic bank Kelvin Winfild ,alisema , Taasisi hiyo ya kifedha moja ya majukumu yake ni kushirikiana na jamii kutoa sehemu ya pato lake ambapo Hadi Sasa imeshatoa kiasi cha sh.Bilioni moja kusaidia katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu na afya.
Alieleza kwa upande wa watoto katika Taasisi hiyo ipo nao pamoja , kwa miaka 20 na kuanzia 2018 walianza ujenzi wa madarasa mawili baada ya majengo ya Taasisi hiyo kubolewa Kimara ili kupisha upanuzi wa barabara.
Winfild alisema ,kwasasa wanakabidhi madarasa kumi kati ya Madarasa hayo, mawili yapo kwenye ukamilishaji.
"Upungufu wa madawati ,sisi Stanbic tulizindua kampeni ya kutoa madawati 1,000 kila mwaka nchini, na Katika kuunga mkono Taasisi hii ya Watoto wetu Tanzania tutawapa madawati 100".
Kwa upande wake , Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Watoto Wetu Tanzania, Evance Tegete alisema lengo la asasi hiyo Ni kuokoa, kuwalinda na kuwaendeleza watoto wenye Mazingira magumu, waliokuwa wakifanyishwa kazi katika madanguro,kazi za ndani , mashambani,walio lazimishwa kuolewa,na watoto waliotelekezwa.
Tegete alisema, toka kituo kianze kimesaidia watoto 368 kati Yao 38 wamemaliza degree ,akiwemo binti ambae alikuwa akifanyishwa kazi na Sasa anategemea kumaliza degree yake ya tatu ya sheria .
Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo, Rais Mstaafu Awamu ya nne, dkt.Jakaya Kikwete alimuelekeza mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge kukaa na walimu wakuu wa Sekondari ili kujitafakari taaluma ya mkoa na kuangalia sababu zinazosababisha kutofanya vizuri zaidi kwenye Sekondari na shule za msingi .
Alisema elimu Ni ufunguo wa Maisha ,jamii inatakiwa kuthamini elimu ya watoto wetu kwa manufaa Yao ya baadae.
Hata hivyo, Jakaya aliwapongeza Stanbic kwa msaada wa kutoa Jumla ya madarasa 10 ambapo nane yamekamilika na mawili yakiendelea kukamilishwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.