Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo amezitaka Taasisi zote za Serikali Mkoani hapo kuandaa na kuratibu ahadi zote zilizotolewa na Viongozi wa Kitaifa na zile zilizo kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
"Barabara zote ambazo ni ahadi za Mhe Rais zitekelezwe, sisi tutashirikiana na Chama cha Mapinduzi kuorodhesha ahadi zote na Kumkumbusha katibu wa Rais. Alisema Ndikilo.
Hayo ameeleza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Bodi ya barabara ya mkoa pwani ambapo kabla ya kikao hicho cha alitembelea baadhi ya Barabara kuona utekelezaji wa Ilani ya CCM na ahadi za Mhe Rais.
Mhe. Ndikilo amesema Mkoa huo unamtandao wa Barabara wa Km 1387.98 zinazo hudumiwa na TANROADS na 5040 zinazo hudumiwa na TARURA. Ameeleza kuwa bajeti ya Barabara ya Mkoa kwa mwaka 2020/21 ni bilioni 35.317 kwa TANROADS na TARURA ni Bilioni 11.245,
"Ukiangalia mtandao wa Barabara na bajeti hizi bado bajeti ni ndogo kulinganiasha na mtandao wa Barabara tulio nao".alisema Ndikilo
Bodi hiyo imeazimia bajeti ya TANROADS na TARURA iwe kwa magawanyo wa asilimia 60 kwa asilimia 40, ili kuwezesha TARURA kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Kupitia kikao hicho cha Bodi ya Barabara Ndikilo ameitaka Mamlaka ya Bandari kuharakisha ujenzi wa Gati eneo la Kilindoni Mafia kwa kuwa tayari kivuko kimekamilika ili kuwezesha magari na abiria kuvushwa kwa usalama, aidha ameitaka Mamlaka hiyo kuchukua ushauri wa Bodi Barabara ya Mkoa ya kujenga Gati kwenye eneo ambalo litatolewa na Halmashauri ya Mafia ambalo halitaathiriwa na Upepo mkali unaosababisha kupwa na kujaa kwa maji.
Kuhusu Daraja la Mkapa Wilayani Rufiji, Bodi hiyo imeshauri TANROADS kufunga Camera ili kuboresha Ulinzi wa daraja Hilo na kubaini watu wanaoweza kuhujumu Taa za Daraja hilo.
Bodi hiyo imeazimia kuwa Viongozi watoe elimu kwa Wananchi wanaodai fidia kupokea malipo yao pale ambapo fedha hizo zinatolewa kwa awamu.
Ndikilo ameitaka TARURA kushirikisha Baraza la Madiwani kuhusu mipango na vipaumbele vya ujenzi wa Barabara kwenye Halmashauri husika.
Ndikilo amewataka Wahe. Wabunge wa Mkoa huo kushiriki vikao hivyo kila wanapohitajika ili kujua hoja na changamoto za Mkoa ili kuzisemea Bungeni na kuwasilisha kwa Wahe. Mawaziri wenye dhamana.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.