Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani limempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira rafiki ya Biashara na Uwekezaji katika mkoa huo.
Salaam za pongezi hizo zimetolewa leo Machi 6, 2024 kwenye Mkutano wa Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani lililofanyika kwenye ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa huo zilizopo Kibaha.
Akiongoza utoaji wa salaam hizo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge ameeleza kuwa Mafanikio ya Uwekezaji katika Mkoa huo yanatokana na jitihada za Mhe. Rais Samia.
Katika mkutano huo, Kunenge amepongeza sekta binafsi kwa kutimiza wajibu wao na kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya Biashara.
Ametoa takwimu kuwa Mkoa una viwanda 1533, viwanda kati ya hivyo 32 vikubwa vimejengwa ndani ya kipindi cha Mhe. Rais Samia huku vingine 25 vikiwa katika hatua mbalimbali za Ujenzi.
Amebainisha kuwa changamoto ya umeme inakwenda kuwa historia akisema "Muda mchache mtakwenda kupata umeme wa kutosha na wawekezaji watapanua Uwekezaji wao, kila mwekezaji atoe takwimu za mahitaji ya umeme kwenye eneo lake."
Amesema kuwa Ujenzi wa Barabara kuelekea maeneo ya uwekezaji na viwanda unaendelea na ametaka wawekezaji kuelekea kuwekeza kwenye maeneo hayo.
Amewataka Watendaji Mkoani Pwani kuwa na wajibu kutafuta wawekezaji na kuelezea fursa za uwekezaji zilizopo Badala ya kusubiri kufuatwa na wawekezaji.
Ameeleza kuwa wawekezaji wengi wanaokuja kuwekeza Mkoani Pwani ni wa Kimataifa na hivyo lazima wapatiwe huduma nzuri, kwa lugha nzuri na rafiki.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.