Waziri wa Ujenzi Mhe Innocent Bashungwa leo amefanya ziara katika Wilaya ya Rufiji na Wilaya ya Kibiti pamoja na mambo mengine amegawa hati za kimili 136 kwa wafugaji kwa ajili ya Mradi wa uwanzishajwi wa Ranchi ndogo Wilayani humo, hatua hiyo ya Ugawaji wa Hati hizo ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya Mhe Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji.
Aidha Mhe Bashungwa amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge pamoja na uongozi wa Wilaya ya Rufiji kwa kutenga maeneo kwa ajili ya uwanzishwaji wa Ranchi Ndogo na kuagiza kuandaa maeneo zaidi ili kutatua kabisa migogoro ya wakulima na wafugaji.
Aidha kupitia mpango huu wa Ranchi ndogo na uboreshaji wa malisho na maeneo ya machunga utaongeza kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa malisho ya Kutosha ya Mifugo
Repoti ya Mradi huo ilioandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kibiti Bibi Hanan Faragih inasema vijiji 18 tayari vimetenga ekari 31,115 sawa na Ha 12,446 za maeneo ya marisho baada ya kufanya mpango wa matumizi Bora ya Ardhi ambapo ngo'mbe mmoja mwenye wastani wa kilo 450 anachukua heka 1 kwa mwaka kwa ajili ya marisho.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wafugaji wa Wilaya ya Kibiti ameishukuru Serikali kwa uwanzishwaji wa Mradi huo kwani utatokomeza ufugaji wa kuhamahama na kuwezesha watoto wanatoka familia za kifugaji kupata Elimu.
Mpango wa uwanzishwaji wa Ranchi ndogo unalenga kudhibiti viashiria vya migogoro Kati ya wafugaji na watumiaji wengine wa Ardhi na utaweza Kuboresha upatikanaji wa maji, malisho ya Mifugo na miundombinu ya Msingi ya Mifugo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.