Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge ameagiza kuanza Ujenzi wa Wodi ya Wazazi katika Zahanati ya Kata ya Mbwawa.
"Wananchi wana kero ya ukosefu wa wodi ya Wazazi kwenye Zahanati hii wanatembea umbali mrefu kilometa 13 kwenda kituo cha Afya kujifungua. Naelekeza Ujenzi wa wodi ya Wazazi uanze mara moja.
"Kituo cha Afya kitachukua Muda kujengwa Zahanati hii ifanyiwe maboresho kwa kujengwa wodi ya wazazi" Ameeleza Kunenge.
Kunenge ameyasema hayo leo Julai 27 2022 alipofanya ziara Halmashauri ya Mji wa Kibaha katika Kata ya Mbwawa kusikiliza na kutatua Kero za Wananchi.
Kunenge ameagiza kutumika kwa Shilingi Milioni tisa 9 zilizotokana na Mauzo ya Trekta ya Mtaa huo katika kuanza Ujenzi wa Wodi hiyo ya Wazazi.
Kunenge amewaelekeza Wananchi kwa kushirikina na Serikali ya Wilaya kutafuta Eneo kubwa la Ujenzi wa Kituo cha Afya.
"Tutafute Eneo muafaka eneo ambalo Wananchi watafika kwa urahisi kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Afya ambacho tayari Serikali imetutengea Takribani Bilioni 2 kwa ajili ya Ujenzi na vifaa tiba" Ameeleza Kunenge.
Akijibu kero nyingine ya Wananchi kusumbuliwa na Kikundi wahalifu kinachojiita Panya teleza katika Barabara ya Visiga madafu Mbwawa Kunenge amesema Panya teleza Waache Mara moja,
"Wasicheze na Serikali kazi ya Serikali ni kulinda uhuru wa Wananchi wake". Amemwagiza kamanda wa Polisi Mkoa kuhakisha wanakomesha Kikundi hicho
"Nisisikie panya teleza shughulikeni nao msionee mtu lakini hakuna mwenye haki ya kuhatarisha usalama wa Mtu mwingine" Ameeleza Kunenge.
amewataka Wazazi kuongea na vijana wao ili wawe na maadili mema.
Kuhusu kero ya ukosefu Ajira na miradi kwenye Kata amemwelekeza Mkurugenzi wa mji kugawa mikopo ya Asilimia 10 Makundi Maalumu ya Wananchi wa kata hiyo. Aidha amewataka vijana kujituma na kufanya kazi kwa bidii wanapopata fursa hizo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.