Coast City Marathon (2023) awamu ya pili kwa kushirikiana na hospital ya Rufaa ya mkoa Tumbi,imekusanya zaidi ya milioni kumi kati milioni 240 zinazohitajika kwa ajili ya ujenzi wa jengo la mama na mtoto hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani, Tumbi.
Mratibu wa mbio hizo, Dk. Frank Muhamba akizungumza leo Novemba 11,2023 kwenye ufunguzi alieleza, mbio hizo ni sehemu ya uhamasishaji wa zoezi la uchangiaji fedha ili kufanikisha ujenzi wa jengo.
Mganga Mkuu wa hospitali ya Rufaa ya Tumbi, Dk. Amani Malima aliwaomba ,wadau mbalimbali zikiwemo Taasisi binafsi na Serikali kujitokeza kufanikisha zoezi hilo.
"Kukamilika kwa jengo hili kutasaidia kupunguza vifo vya uzazi na watoto , pia hospital hii kwasasa Serikali imeboresha huduma za afya tunatoa huduma ya kusafisha figo ,CTScan na kutoa ujuzi kwa wataalamu wa afya ambapo kwa siku tunahudumia wagonjwa wa kawaida 500 na wodi ya uzazi 200 katika hospital yetu, idadi ambayo ni kubwa" alifafanua Malima.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa afya, Ummy Mwalimu, Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge,alisema katika kuunga mkono juhudi za ujenzi wa wodi ya mama na mtoto ofisi ya mkoa huo imetoa sh milioni tano.
Alifafanua kuwa, hospitali ya Rufaa ya Tumbi ilipewa hadhi ya kuwa rufaa mwaka 2011 na inahudumia wagonjwa kutoka wilaya sita za mkoa huo na mikoa jirani, Dar es Salaam, Tanga na Morogoro.
“Kwa sasa hospitali ya Tumbi inapokea wagonjwa 500 kwa siku na 2,081 kwa mwezi ,ni hospital kubwa katika mkoa ya Serikali ,inaendelea kushirikisha na wadau mbalimbali ili kuchangia ujenzi wa miundombinu na vifaa tiba,”anaeleza Kunenge.
Hospital ya rufaa ya mkoa ya Tumbi, inapokea akinamama katika wodi ya uzazi wapatao 24,000 kwa mwaka ,na 200 kwa mwezi ,ikiwa na pamoja na vitanda vitatu vya kujifungulia na vitanda 24 vya kulaza katika wodi hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.