Mkuu wa Wilaya ya ya Kibaha, Mhe. Nikson Simon, amesisitiza umuhimu wa upendo katika utekelezaji wa majukumu ya watumishi wa Mahakama Mkoa wa Pwani ili kuhakikisha haki inatendeka wakati wa kushughulikia kesi za wananchi.
Nickson alitoa kauli hiyo Februari 3, 2025 wakato wa madhimisho ya kilele cha siku ya sharia nchini ambapo alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhe . Abubakar kunenge . Maadhimisho hayo ambayo yalifanyika katika Viwanja vya Mahakama ya Hakim Mkazi Kibaha yaliyobeba kauli mbiu "Nafasi ya Taasisi zinazosimamia Haki na Madai Katika Kufikia Malengo Makuu ya Dira ya Maendeleo."
Akihimiza maadili mema kwa watendaji wa mahakama , Nickson alisema “Kupenda kunafanya kuwa tayari kusimamia sheria na kupinga uovu. Tuwe na upendo kwa watu tunawahudumia, na mtu mwenye upendo hawezi kupora haki, hivyo nasisitiza kuwa na upendo ili tuweze kutenda haki”.
Aidha, aliwataka wadau mbalimbali na wananchi kutii sheria, akisema, "Sheria ni sisi na sisi wote ni sawa mbele ya sheria. Tukiboresha sheria, tumejiboresha sisi, na tukiharibu, tumejiharibu sisi."
Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha, Mhe. Joyce Mkhoi, aliwataka wadau mbalimbali kutoa maoni katika rasimu ya Dira Mpya ya Maendeleo ya Taifa ya 2050, kwani ndiyo msingi wa kukuza maendeleo na uchumi wa nchi.
Alisema pia kuwa Siku ya Sheria Nchini, inayoadhimishwa kila mwaka, ilitanguliwa na Wiki ya Sheria, ambayo ilikuwa ni wiki ya utoaji elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya Mahakama na Sheria kwa ujumla. Wiki hiyo ilianza tarehe 25 Januari na kumalizika tarehe 01 Februari mwaka huu, ikiwa imefanyika katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ofisi za serikali, shule za msingi, sekondari, maeneo ya wazi, na ofisi za serikali za mitaa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.