Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, ambaye pia ni Skauti Mkuu Tanzania, Rashid Mchatta, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera.
Dkt. Serera yupo mkoani hapa kwa ziara ya siku moja katika Kiwanda cha Viuatilifu cha Tanzania Bio-Tech kinachosimamiwa na Shirika la Maendeleo la NDC.
Katika mazungumzo yao, Katibu Tawala Rashid Mchatta ameelezea changamoto mbalimbali zinazokumba sekta za viwanda na uwekezaji, hususan tatizo la upatikanaji wa nishati ya gesi, ambayo ingeweza kusaidia kuboresha uzalishaji viwandani.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Serera aliahidi kushughulikia changamoto hizo zilizowasilishwa na uongozi wa mkoa.
Aidha, Dkt. Serera amepongeza Serikali ya Mkoa wa Pwani kwa kusimamia kwa ufanisi ajenda ya maendeleo ya viwanda, hatua iliyochangia Mkoa wa Pwani kuongoza kwa kuwa na viwanda vingi zaidi nchini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.