Mkoa wa Pwani umetunukiwa cheti na kikombe maalum kwa kuwa Mkoa mwenyeji wa Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2025, huku Halmashauri ya Chalinze ikiibuka mshindi wa kwanza wa mbio hizo katika Kanda ya Nne inayojumuisha mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara, Kigoma, Katavi na Rukwa.
Akizungumza katika sherehe za kuhitimisha Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika leo, Oktoba 14, 2025, katika Viwanja vya Sokoine, Jijini Mbeya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb), alisema kuwa tuzo hizo zimetolewa kwa mikoa iliyozindua na kufanikisha kilele cha mbio hizo pamoja na Halmashauri zilizofanya vizuri.
Aidha, Halmashauri zilizoshinda katika ngazi za kanda zimetunukiwa Cheti, Kikombe na zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni tano (Tsh 5,000,000) kwa kila mshindi, ikiwa ni sehemu ya kutambua juhudi zao katika kuibua, kutekeleza na kusimamia miradi yenye tija kwa jamii kupitia mbio hizo za Mwenge wa Uhuru.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.