Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Dkt Delphine Magere ,amewataka watumishi katika Ofisi yake kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi na kuzingatia taratibu za utumishi wa umma.
Akiwa katika kikao cha kawaida na watumishi hao Dr. Magere aliwaasa watumishi hao kushirikiana katika kufanya kazi ili kuleta tija.
“Natarajia kuona mnashirikiana katika kila jambo hapa kazini na kila mmoja wenu afanye kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za Utumishi wa umma, tukizingatia haya yote tutafika mbali” alisema Dkt Magere.
Kuhusu mahudhurio kazini, DKt Magere aliwataka watumishi wote kuwahi kufika kazini kwa wakati na kila mtumishi ahakikiahe kuwa anajisajili katika mfumo wa mahudhurio wakati akiingia na kutoka kazini.
Mbali na hayo Dkt Magere ametaka watumishi hao kuhakikisha kuwa wanajituma kwa bidii katika utendaji wa kazi yao ili kufanikisha malengo ya Mkoa.
Hiki ni kikao cha Kwanza kwa Katibu Tawala huyo kukutana na watumishi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani na kuelezea matarajio yake ya kiutendaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.