Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amemtaka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini Tanzania (TARURA) Mkoa wa Pwani kuhakikisha Miradi ya Barabara wanayoisimamia Mkoani Hapo inakamilika kwa wakati.
Ndikilo aliyasema hayo leo Desemba 15,2020 wakati alipofanya ziara kukagua baadhi ya Miradi ya Barabara kwenye Wilaya za Kibaha na Bagamoyo.
katika ziara hiyo Ndikilo amekagua Ujenzi wa Barabara ya TAMCO -Mapinga yenye urefu wa Kilometa 23, akiwa katika Mradi huo Ndikilo amemtaka Meneja wa TANROADS kusimamia Mkandarasi aliyepatikana kuanza ujenzi kipande cha Mita 600 kwa haraka. Barabara hiyo inajengwa kwa awamu hadi sasa zimejengwa Kilometa 2.9 kwa kiwango cha lami na kubaki Kilometa 20.1. Aidha, Amemtaka Mratibu wa TARURA Mkoani hapo kuandaa mpango wa Kujenga barabara ya mzunguko (Roundabout) kwa kiwango cha changarawe katika makutano ya barabara za NIDA -Loliondo Mjini Kibaha na kuwasilisha mpango huo siku ya kikao cha Bodi ya Barabara tarehe 22 Desemba 2020, Ndikilo amefikia uamuzi huo baada ya TARURA kueleza kuwa hawana fedha kiasi cha shilingi Milioni 400 za kujenga roundabout hiyo kwa sasa hadi Julai 2021." Hatuwezi kukaa zaidi ya mwaka mmoja na kupaacha eneo hili bila matengenezo, hapa ni katikati ya Mji tuje na mpango wa kuparekebisha kwanza kwa kiwango cha changarawe kabla ya kupata fedha hizo" alisema Ndikilo.
"Barabara ya TAMCO- Mapinga ni ahadi ya Mhe Rais wakati wa Kampeni alipokuja Mkoani kwetu na ipo kwenye Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndani ya Kipindi cha miaka 5 tunauhakika Barabara hii itakamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, Barabara hii ni ya muhimu kwa kuwa eneo hili lina ardhi kwa ajili ya Ujenzi wa Viwanda ikikamilika itavutia wawekezaji, ni njia rahisi ya kuunganisha Makao Makuu ya Mkoa Kibaha na Wilaya ya Bagamoyo" ameeleza Ndikilo. Amesema kuwa Ujenzi wa Barabara hiyo utapelekea kuwepo kwa usafiri wa uhakika na hivyo kusaidia Wanafunzi na jamii ya kuondokana kero ya kutembea umbali mrefu.
Akiwa kwenye Barabara ya kuelekea kwenye eneo la Viwanda la Zegereni (Visiga -Zegereni) Kibaha yenye urefu wa kilometa 12 ameeleza kuwa barabara hiyo inaharibika mara kwa mara wakati wa mvua. "Wenye viwanda wamekuwa wakilalamika kuwa wanashindwa kutoa bidhaa viwandani kwenda sokoni ambapo kuna viwanda vikubwa 25 Vinavyofanya kazi kwenye eneo hilo, kwa kuwa serikali inahimiza ujenzi wa viwanda na wadau wameitikia wito wa ujenzi wa viwanda lazima tuhakikishe tunawawekea mazingira mazuri kwa kujenga barabara ili zipitike na kuwaondolea kero ya kusafirisha bidhaa na malighafi kwenda viwandani na sokoni,”alisema Ndikilo.
"Mpango wa Serikali ya Mkoa ni kuhakikisha barabara hii inapitika mwaka mzima ili wenye viwanda wanaposafirisha malighafi kwenda viwandani na kutoa bidhaa kupeleka sokoni wasafirishe kwa muda mfupi" nimemuona mkandarasi yupo eneo la mradi anatengeneza maeneo korofi, habari njema ni kwamba Serikali pia imetoa fedha shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa kilometa moja ya lami ya barabara hii" alisema Ndikilo.
Akikagua Barabara ya Kwa Mathias, Nyumbu Msangani (Kibaha) yenye Urefu wa Km 8.5, amewathibitishia Vikosi vya Jeshi Kamandi ya Nchi kavu, Shirika la Nyumbu na wananchi wa eneo hilo kuwa wanaendelea kujenga kwa awamu hadi kukamilisha kilometa zote 8.5. "Niwapongeze TANROADS kwa kujenga Km 2.32 kwa kiwango cha lami kwani kabla ya ujenzi huo magari na usafiri ulikuwa mgumu eneo hili" kwa sasa TANROADS tayari wamepata mkandarasi na wataanza ujenzi wa M 600 hadi geti la Shirika la Nyumbu. " nimeridhika na kiwango kilichojengwa rai yangu ni kwa mkandarasi anyaejenga hizi M 600 kufanya haraka na kukamilisha ndani ya miezi 8 iliyopangwa.
Akikagua Ujenzi wa barabara Eneo Korofi la Vigwaza, amepongeza Ujenzi huo na kusema kuwa Uboreshaji wa maeneo korofi utasaidia kuepusha ajali kutokea na kuboresha usalama na hali ya barabara,"Barabara ya Morogoro ni ya Muhimu sana inasafirisha abiria na mizigo kwenda mikoani na Nchi jirani, mara nyingi pamekuwa pakiharibika na kusababisha msongamano, nimefurahi kusikia baada ya siku is mbili mtafungua magari yataanza kupita hapa Vigwaza kazi you ni nzuri" alisema Ndikilo.
Ndikilo ametembelea pia ujenzi wa Barabara ya Vigwaza-Bandari kavu ya Kwala yenye to urefu wa km 15.5 inayojengwa kwa kiwango cha zege, amepongeza ujenzi huo unaogharimu bilioni 30 na half kumtaka Mkandarasi kufanya is kazi is usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi huo, amezitaka Mamlaka ya Bandari TPA kuhakikisha inawalipa fidia wananchi waliopisha mradi huo you ifikapo Januari 15, 2020. Amewataka wawekezaji kuchangamkia fursa ya ujenzi wa Viwanda na uwekezaji mwingine kwenye eneo hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.