Hayo yamebainishwa Me i29 2020 wakati wa baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo lililofanyika kujadili hoja za taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa fedha 2018/19.
Akizungumza katika baraza hilo
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo, ameipongeza Halmashauri hiyo kupata hati safi kwa Miaka minne mfululizo.
Aidha, ameitaka Halmashauri hiyo kujibu Hoja zote za Ripoti hiyo ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali ndani ya siku 14
"Ninaa giza kufungwa kwa hoja zote 38 zikiwemo Ile 11 za miaka ya nyuma ambazo zipo ndani ya uwezo wa Halmshauri ndani ya siku 14 “ alisema Mhandisi Ndikilo.
Amewataka Viongozi wa Halmashauri hiyo kuepuka kuzalisha Hoja na kutaka watendaji kuzingatia sheria, kanuni na taribu.
Pia ameitaka halmashuri hiyo kutumia vizuri kitengo cha ukuaguzi ikiwa njia moja wapo ya kuepuka hoja hizo .
Ndikilo ametumia baraza hilo kuitaka Halmashauri hiyo kubuni mbinu mpya za Ukusanyaji wa Mapato pamoja na kutumia bandari ya nchi kavu ya Kwala katika kukusanya mapato.
Nae kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha bi Asumpter Mshama ameipongeza halmashauri hiyo na ameitaka kuwekeza zaidi katika Elimu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.