Hayo yamesemwa leo Juni 3 2020 na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani Mkuranga cha kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Mwaka 2018/19.
"Halmshauri ya Wilaya ya Mkuranga ni Halmshauri nyeti kwa uchumi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla" alisema Ndikilo
Ndikilo amesema takwimu za ukusanyaji mapato ya TRA kwa mwaka 2019 hadi Mei 2020 Wilaya ya Mkuranga imekusanya Bilioni 14.46 Katika lengo la Mkoa la Bilioni 51 kufanya Wilaya hiyo kichangia asilimia 28.2 ya mapato yote ya Mkoa.
Mapato ya Ndani (Own Source) 2019/20 lengo ni Bilioni 6.31 kiasi kilichokusanywa mpaka Mei 2020 ni Bilioni 5.99 sawa na asilimia 95%
Ndikilo ameendelea kuitaka Halmashauri hiyo kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuthibiti upotevu vya mapato kwenye vyanzo vilivyopo ikiwemo chanzo cha mchanga.
Katika hatua nyingine
Ndikilo ametoa siku saba kwa watumishi waliokuwa wakikusanya mapato kwa njia ya mashine za POS kuwasilisha fedha hizo.
Ndikilo alimtaka pia Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filberto Sanga kumpatia majina ya waliohusika na ukusanyaji wa mapato na kushindwa kuwasilisha fedha shilingi 150 kwa Halmashauri.
“Hata kama ni mtumishi wa Serikali lazima arudishe fedha za Umma, Mkuu wa Wilaya nipatie majina ya wale waliokuwa wakihusika na kukusanya mapato hayo alisema Ndikilo.
Alisema, wahusika wanatakiwa kurejesha fedha hizo huku hatua za kisheria dhidi yao zikiendelea kuchukuliwa lengo kutoa fundisho kwa wengine.
Mkuu huyo wa Mkoa alitoa wito kwa Mkurugenzi na Baraza hilo la Madiwani kuepuka kutoa mikataba mibovu kwa mawakala wa ukusanyaji wa mapato.
Katika hatua nyingine Mhandisi Ndikilo alipongeza Halmashauri hiyo kwa kupata hati safi kwa miaka minne mfululizo huku akitoa agizo kwa Mkaguzi wa Ndani wa Halmshauri hiyo kuzuia uzalishaji wa Hoja.
Aidha alitaka hoja za miaka ya nyuma ambazo Halmashauri ina uwezo wa kuzishughulikia zifungwe mapema ndani ya siku 90.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.