Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,ambae pia ni mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega ameeleza lengo la ongezeko la idadi ya watalii milioni 5 na kuzalisha dollar za kimarekani Bilioni 6 ifikapo,2025 itawezekana kutokana na ongezeko la watalii kwa sasa.
Akitembelea baadhi ya mabanda ya washiriki wa maonyesho ya wiki ya biashara na uwekezaji Mkoani Pwani yanayofanyika Mailmoja Kibaha Mjini,Ulega akiwa banda la Wizara ya Utalii pamoja na banda la Halmashauri ya Mafia na Mkuranga alisema ,namna idadi inavyoongezeka na kuingiza dollar bilioni sita kufikia 2025 inawezekana .
"Inabidi tushirikiane ,tufanyekazi ,tuwe wabuni ,umoja na kupanua wigo wa kujitangaza ili kuongeza watalii nchini na kuinua Pato la Taifa hadi lifikie asilimia 30-40 na hii kwa juhudi zetu Tutafika"Hakuna kinachoshindikana inawezekana."alifafanua Ulega.
Ulega alieleza ,Hifadhi za Taifa ikiwemo Ngorongoro,Saadan ,Selou,na Vikindu Forest zifanye kazi ili kuvutia watalii ndani na nje ya nchi.
Aidha akitembelea Banda la Halmashauri ya Mkuranga aliwataka kufanya marejesho ya tamasha la Utalii Mkuranga ambalo lilileta matokeo chanya.
Ulega alifafanua kwamba ,Vikindu forest iliyopo Mkuranga ni utalii tosha ambapo kwasasa watalii 500 wanafika kujionea vivutio mbalimbali na wengine kwenda kupumzika kwa mwezi .
"Hii ni hatua nzuri ya uwekezaji endeleeni kupaendeleza ili kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje "
Wakati akiwa Banda na Halmashauri ya Mafia ,Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mohammed Hussein aliwashawishi watu waende Mafia kujionea kivutio kikubwa Cha Papa Potwe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.