Jeshi la Wananchi wa Tanzania limetoamagari kumi kwa ajili ya kusaidia kusafirisha vyakula kwenda kwenye makambi yawaathirika wa mafuriko walioko kwenye Wilaya za Rufiji na Kibiti Mkoa wa Pwani.
Akipokeamagari hayo April 18, 2024 wilayani Rufiji, Mkuu wa Mkoa wa Pwani AbubakarKunenge amempongeza Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naMkuu wa Majeshi kwa magari hayo.
Ameelezakuwa wamepata misaada ya vyakula lakini kulikuwa na changamoto ya usafiri naBarabara katika kufikia walengwa.
Amesemamagari hayo yatasaidia kufika kirahisi maeneo hayo yenye changamoto.
VilevileKunenge amepongeza Jeshi kwa kuendelea kulinda mipaka ya nchi na Amanikuendelea kuhudumia Jamii.
KadhalikaKunenge,amekabidhi magari hayo kwa Wakuu wa Wilaya za Kibiti na Rufiji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.